Gitega : majaji saba wapelekwa jela

Gitega : majaji saba wapelekwa jela

Majaji saba wanazuiliwa katika gereza kuu ya Gitega (mji mkuu wa kisiasa) tangu alhamisi jioni, mashahidi walithibitishia SOS Médias Burundi. Wanatuhumiwa vitendo vya rushwa na utapeli. HABARI SOS Médias Burundi

SOS Médias Burundi ilifanikiwa kupata utambulisho wao. Majaji hao ni pamoja na : Désiré Manirakiza naibu wa kwanza wa mwendeshamashtaka katika mkoa wa Karusi ( mashariki ya kati mwa nchi ) Renovat Manirampa, jaji katika mahakama ya rufaa ya Gitega ( mji mkuu wa kisiasa) , Janvier Nizigiyimana jaji katika mahakama hiyo , Philotaire Ndayishimiye jaji katika korti mkuu ya Gitega , Floridas jaji katika mahakama ya rufaa ya Gitega, Abel Irankunda mfanyakazi wa idara ya sheria katika gereza kuu ya Gitega pamoja na Nestor jaji katika korti kuu ya mkoa wa Gitega.

Mfungwa wa nane ni Jean Masabarakiza, mfanyakazi mdogo katika mahakama ya jamuhuri mkoani Gitega.

Kwa mjibu wa vyanzo katika idara ya sheria, wanatuhumiwa makosa mawili : utapeli na rushwa

Sababu za kufuatiliwa

Kwa mjibu wa vyanzo vya karibu na faili hiyo, yote yalitokana na kisa cha kuachilia huru wafungwa.

” Kuna mtu anayejifanya kama dalali. Anawasiliana na familia za wafungwa au na wafungwa wenyewe harafu anakuwa kama mpatanishi kati yao na majaji ili kusaidia faili zao zishughulikiwe haraka au waachiliwe huru. Ili kuwakubalisha wateja wake, anawatumia ujumbe wa sauti uliorikodiwa wakati wa mazungumzo na majaji”, vyanzo katika idara ya sheria mkoani Gitega vinasema.

” Ushahidi unaomilikiwa na waendesha mashtaka ni ujumbe wa sauti uliorikodiwa wakati wa mazungumzo kwenye simu”, vyanzo vyetu vinaeleza.

Vyanzo vinaendelea kuwa kikao cha kesi ya mafumanio kwa ajili ya watu hao nane kinaandaliwa .

Mahabusu hao nane walikamatwa alhamisi mchana kwa amri ya mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri. Walipelekwa moja kwa moja ndani ya gereza kuu ya Gitega ambako walihojiwa .

” Wa mwisho alitumwa katika chumba chake cha gereza majira ya saa sita za usiku “, shahidi mmoja alisema.

Kukamatwa kwa dalali

Mtu aliyekuwa chanzo cha kamata kamata hiyo alisimamishwa siku ya ijumaa. Alizuiliwa katika jela la polisi ndani ya mji mkuu wa kisiasa, kwa mjibu wa vyanzo vya polisi.

Hadhi ya kukatiwa kesi

Ni korti kuu ambayo ina kiwango cha kushughulikia kesi ya mahabusu hao nane. Majaji nchi Burundi wana kinga ya kuhukumiwa.

Kwa mjibu wa vyanzo mbali mbali, wafanyakazi wengine takriban 10 wa sekta ya sheria mashariki ya kati nchini Burundi wako kwenye orodha ya wale wanaotakiwa kukamatwa.

Previous Tanzania : viongozi wanahakikisha kuwa unyanyasaji dhidi ya wakimbizi wa Burundi unapuziwa
Next Bubanza : shambulio la waasi kwa silaha kutoka DRC katika eneo la Buringa