Bubanza : shambulio la waasi kwa silaha kutoka DRC katika eneo la Buringa

Bubanza : shambulio la waasi kwa silaha kutoka DRC katika eneo la Buringa

Milio ya silaha nzito na kawaida ilisikika jumamosi jioni katika kijiji cha Buringa, tarafani Gihanga mkoa wa Bubanza (magharibi mwa Burundi). Waasi huenda walitoka katika mbuga ya Rukoko kwenye mbambao wa mto wa Rusizi unaotenganisha Burundi na jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Kundi la silaha la Red Tabara lenye asili ya Burundi lililopiga kambi Kivu ya kusini (mashariki mwa DRC) lilidai kuhusika na shambulio hilo. Kulingana na matokeo ya muda, ni watu wawili waliouwawa na mwingine kujeruhiwa. Vifaa vingine vilivyoharibika ni vingi. HABARI SOS Médias Burundi

Jumamosi majira ya saa 3:30 usiku mripuko ya guruneti na milio ya risasi vilisikika katika kijiji cha Buringa.

Kwa mjibu wa wakaazi wa eneo hilo, lilikuwa kundi la watu waliokuwa na silaha nyingi.

” Kwanza walilenga gari iliyokuwa ikielekea Bujumbura ( mji mkuu wa kisiasa) gari hiyo iliteketea kwa moto mara moja. Mmoja kati ya abiria aliungua na moto. Mwingine aliuwawa kwa kupigwa risasi. Mabaki ya gari hiyo yaliondolewa na wajumbe wa vikosi vya usalama”, alisisitiza.

Waasi hao walitoboa kwa risasi gari nyingine iliyokuwa imeegeshwa.

Mmiliki wa gari hiyo ni Éric Badogo mkaazi wa Buringa . Walilenga pia pikipiki ambayo iliharibika Waasi hao walivurumisha guruneti ndani ya mgahawa na kuondoka baada ya vikosi vya usalama kuingilia kati “, alithibitisha mkaazi mwingine wa makao makuu ya Buringa.

Wakaazi wa eneo hilo wanalaani shambulio hilo lililofanyika huku mbuga hiyo ya Rusizi ikiwa inalindwa na wanajeshi usiku na mchana.

” Kutokana na shambulio hilo, hakuna kinachoweza kutuhakikishia, usalama wetu unaweza kuvurugika wakati wowote”, ni wasi wasi wa mkaazi mmoja.

Ma kumi ya askali polisi na wanajeshi walitumwa eneo hilo hadi jumapili asubuhi. Walihakikisha kuwa wamefanikiwa kumuondoa aduwi.

Polisi na viongozi eneo hilo bado hawajajieleza kuhusu shambulio hilo lakini ujumbe wa hali ya juu umewasili eneo la tukio, afisa wa chuo katika polisi eneo hilo amethibitishia SOS Médias Burundi.

Red Tabara ni kundi la silaha lenye asili ya Burundi lililopiga kambi Kivu kusini. Kundi hilo linachukuliwa na viongozi wa Burundi kama kundi la kigaidi. Limedai kutekeleza shambulio hilo

Kwenye mtandao wa X maarufu kama Twiter , kundi hilo limefamisha kuwa ” limeharibu mtambo wa kuelekeza ndege zinazokaribia kutuwa kwenye uwanja wa ndege wa Bujumbura ambao unapatikana eneo la Gihungwe sio mbali sana na maeneo ambapo watu hao wawili wameuwawa.

” Wapiganaji wa Red Tabara wanaopatikana nchini Burundi wanaweka kutekeleza shambulio mahala popote na wakati wowote ” limesema kundi hilo la silaha. Lakini jumapili hii, rais Ndayishimiye pamoja na mkeo wametumia uwanja huo kuelekea Nairobi ambako kutafanyika mkutano kuhusu mazingira.

Juni iliyopita, wakaazi walitoa taarifa kuhusu uwepo wa watu wa silaha walioingia katika msitu wa Kibira. Walitumia kijiji hicho.

Tangu mwaka wa 2015, watu wa silaha kutoka DRC wanajaribu kudhibiti msitu wa Kibira kutoka eneo hilo. Majaribuo yao yanashindwa hadi wakati huu.

Previous Gitega : majaji saba wapelekwa jela
Next Nyarugusu (Tanzania) : misaada yasimamishwa kwa wakimbizi zaidi ya 200 wenye uraia wa Burundi wanaotembea na ulemavu