Kayogoro : wafuasi wa vyama vya upinzani watiwa wasi wasi na sensa inayofanyika

Kayogoro : wafuasi wa vyama vya upinzani watiwa wasi wasi na sensa inayofanyika

Wafuasi wa vyama vya upinzani wanasema kuwa wanahofia mabaya kutokea kufuatia sensa iliyoanza jumatano tarehe 7 juni katika kijiji vyote vya tarafa ya Kayogoro mkoa wa Makamba (kusini mwa Burundi) . Sensa hiyo ya wananchi kuhusu vyama vyao inaendeshwa na wafuasi wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD Imbonerakure. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa vyanzo katika tarafa ya Kayogoro, sensa hiyo ilianza jumatano tarehe 7 katika vijiji vyote vya tarafa hiyo.

Sensa hiyo inatofautisha wafuasi wa chama cha CNDD-FDD na wale wa upinzani, jinsia na miaka yao .

Vyanzo vyetu vinathibitisha kuwa Imbonerakure wanaofanya sensa hiyo hupita nyumba hadi nyingine katika vijiji vyote na vitongoji.

Kulingana na vyanzo katika baadhi ya Imbonerakure wanaoendesha sensa hiyo, zoezi hilo linalenga kuwatishia wafuasi wa vyama vya upinzani ili wasithubutu kuonyesha uwanachama wao katika vyama vya upinzani.

” Hiyo itatusaidia kupotosha matokeo ya uchaguzi ujao”, walihakikisha Imbonerakure waliozungumza na SOS Médias Burundi.

” Hiyo itatuwezesha kuhakikisha kuwa hakuna hata mfuasi mmoja wa chama cha upinzani katika vijiji mbali mbali na kwa hiyo chama cha upinzani hakitakuwa na haki ya kupinga matokeo” alifahamisha Imbonerakure mmoja wa eneo hilo kwa sharti ya kubana jina lake.

Upande wa upinzani, wafuasi wanasema kuwa wanaishi katika hali ya wasi wasi kwa sababu ” hali hiyo inaweza kusababisha mauwaji ya wafuasi wa upinzani”.

Wanaomba viongozi wa nchi kusimamisha mara moja aina hiyo ya sensa. Viongozi wa tarafa na wakuu wa chama tawala hawakupatikana ili kujibu maswali yetu.

Previous DRC (Beni) : watu zaidi ya kumi wauwaw a katika shambulio jingine la kundi la ADF eneo la Rwenzori
Next DRC : raia wa Kongo waelekea kupata kadi ya uraia