DRC (Beni) : watu zaidi ya kumi wauwaw a katika shambulio jingine la kundi la ADF eneo la Rwenzori

DRC (Beni) : watu zaidi ya kumi wauwaw a katika shambulio jingine la kundi la ADF eneo la Rwenzori

Watu 13 waliuwawa katika shambulio jingine ya waasi wa AFD (nguvu zilizoungana kwa ajili ya demokrasia) katika usiku wa alhamisi kuamkia ijumaa . Shambulio hilo lilifanyika katika kitongoji cha Bukokoma karibu ya eneo la Nzenga kwenye umbali wa kilometa takriban tano kutoka kijiji cha Mutwanga makao makuu ya Rwenzori ndani ya wilaya ya Beni mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC. HABARI SOS Médias Burundi

Hayo yanaripotiwa na baraza la vijana wa eneo la Rwenzori ambao wanazidi kuhakikisha kuwa mbali na watu waliouwawa, wengine wengi hawajulikani walipo. Mifungo mingi pia iliibiwa .

Kulingana na Bernard Muke, kiongozi wa baraza hilo, waasi waliingia kwa kujificha ndani ya kijiji hicho. Waliuwawa wananchi wa kawaida kwa kutumia silaha zisizokuwa za moto kama wanavyoripoti mashahidi.

” ilikuwa majira ya saa tatu za usiku ambapo adui aliingia katika vijiji vya Bukokoma kuelekea magharibi mwa kijiji cha Mutwanga ambapo walianza kuwauwa wananchi. Majira ya saa saba za usiku katika siku ya ijumaa tarehe 9 juni, tulianza kupata ujumbe kuwa miili ya watu zaidi ya kumi imefikishwa katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali kuu ya Mutwanga. Tukiangalia namna walivyotenda, bila shaka ni waasi wa kundi la ADF waliotekeleza shambulio hilo. Waasi hao walikuwa wakijaribu kuingia katika eneo hilo kwa muda mrefu pasina kufanikiwa. Walibadili mbinu kwa kuingia katika majumba bila kupiga risasi”, alifahamisha.

Baraza la vijana wa eneo hilo la Rwenzori linasema kuwa wananchi wengine wa kawaida huenda walitekwa na waasi lakini pia mali za wananchi ziliibiwa wakati wa uvamizi huo.

Bernard Muke inatoa wito kwa wananchi kuwa wangalifu. Hata hivyo analaani uzembe unaoshuhudiwa tangu siku chache zilizopita upande wa taasisi ya usalama katika eneo hilo. Alizidi kusema kuwa hali hiyo inatoa nafasi kubwa kwa kundi la ADF kuvamia wananchi waliotulia.

Previous Burundi : noti mpya za elfu tano na elfu kumi zawekwa katika mzunguko wa pesa
Next Kayogoro : wafuasi wa vyama vya upinzani watiwa wasi wasi na sensa inayofanyika