DRC : raia wa Kongo waelekea kupata kadi ya uraia

DRC : raia wa Kongo waelekea kupata kadi ya uraia

Mkataba ulitiwa saini alhamisi hii tarehe 8 juni kati ya tume ya kitaifa ya uchaguzi (CENI), ofisi ya kitaifa ya utambulisho na wananchi (ONIP) pamoja na idara ya kitaifa ya takwimu (INS) kwa lengo la kuwapatia wananchi wa Kongo kadi ya uraia. Itakuwa ni mara ya kwanza kwa raia wa Kongo kupewa kadi ya uraia. Waziri mkuu aliyehudhuria sherehe hizo za kutia saini aliwasihi kuteleleza kikamilifu misheni hiyo ” kwa mantiki ya kuweka vitendoni muongozo wa rais wa jamuhuri Félix Tshisekedi”. HABARI SOS Médias Burundi

Mkataba huo unaamuru kwanza tume huru ya kitaifa ya uchaguzi kuzikabidhi ofisi za ONIP na INS data na vifaa ya kukusanyisha maelezo pamoja pia sheria za uandikishaji. Ofisi hizo mbili zinatakiwa kuendelea na operesheni ya utambulisho na sensa ya wananchi na hivyo kufungua njia ya kutoa kadi ya uraia.

Sherehe hizo zilifuatiwa na kukabidhi ofisi ya ONIP alama za baadhi ya vifaa vilivyotumiwa katika zoezi la kuandikisha wapiga kura ili kuruhusu ofisi hiyo kuanzisha rasmi zoezi la kuorodhesha wananchi kwa kuanzia katika mji- mkoa wa Kinshasa kama mkoa wa mfano mnamo siku zijazo.

Mbali na vifaa hivyo, tume huru ya kitaifa ya uchaguzi ilikabidhi kwa muda wafanyakazi wake ofisi hiyo ya kitaifa ya utambulisho wa wananchi ili kuunga mkono zoezi hilo.

Akieleza kuwa kitendo hicho ni kwa lengo la kutumia vizuri uwezo wa kifedha ambao serikali ingetumia ili kutekeleza operesheni hiyo, waziri mkuu Sama Lukonde alitoa wito kwa wadau kuongeza juhudi ili kufikia malengo waliojipa.

Katika nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati, ni kadi ya wapiga kura ambayo hutumiwa kama kadi ya uraia hadi sasa. Kwa sababu hiyo, hata wafungwa wanaorodheshwa wakati wa kipindi cha uchaguzi ili kuepusha wafungwa wa zamani kujikuta wakiwa hawana kadi ya utambulisho.

Previous Kayogoro : wafuasi wa vyama vya upinzani watiwa wasi wasi na sensa inayofanyika
Next DRC (Kivu kaskazini) : shughuli zaanza pole pole kwenye mpaka wa Bunagana