DRC (Kivu kaskazini) : shughuli zaanza pole pole kwenye mpaka wa Bunagana

DRC (Kivu kaskazini) : shughuli zaanza pole pole kwenye mpaka wa Bunagana

Gavana mwanajeshi wa jimbo la Kivu kaskazini Constant Ndima alitangaza kuwa harakati kwenye mpaka wa Bunagana (kati ya Uganda na DRC) ni lazima zianze tena . Eneo hilo liko chini ya udhibiti wa wapiganaji wa kundi la machi 23, M23 tangu mwaka jana. HABARI SOS Médias Burundi

Gavana aliwaomba wajumbe wake kuchukuwa hatua zote zinazostahili ili kupeleka vifaa kwenye mpaka wa Bunagana chini ya ulinzi wa kikosi cha kanda ya EAC.

Ni kwa lengo la kuangalia hali halisi ya huduma mbali mbali na kutoa taarifa kwa viongozi wao.

Alizungumzia hatua hiyo kupitia Tangazo, Willy Ngoma msemaji wa M23 alichukuwa hatua hiyo ya gavana wa mkoa wa Kivu kaskazini kama uchokozi .

Kundi la M23 lilichukuwa tena udhibiti wa eneo hilo la mpakani tarehe 22 julai 2022.

Previous DRC : raia wa Kongo waelekea kupata kadi ya uraia
Next Cibitoke : Zaidi ya wafungwa 180 ndani ya gereza ndogo ya polisi