Nyarugusu (Tanzania) : misaada yasimamishwa kwa wakimbizi zaidi ya 200 wenye uraia wa Burundi wanaotembea na ulemavu
Idadi kubwa ya wakimbizi wenye uraia wa Burundi wanaoishi na ulemavu hawakupata msaada wao wa mkaa. Zaidi ya 200 kati yao hawakuona majina yao kwenye orodha ya wanaohitaji misaada. Wanakosoa ukiukwaji huo mkubwa wa haki zao za msingi. HABARI SOS Médias Burundi
Ni majonzi makubwa kwa wakimbizi wenye uraia wa Burundi wanaoishi na ulemavu, wale wanaosumbuliwa na maradhi yasiopona au wenye umri mkubwa. Sababu : hawako kwenye orodha ya wanaopewa msaada katika miezi ya agosti -septemba.
” Tulihesabu zaidi ya watu 200 ambao hawakupewa mkaa wao wa nishati. Kwa hiyo, jiulize vipi watu wanaotembelea kiti cha kurudumu, wazee wa zaidi ya miaka 70 au wale wanaotembea na virusi vya ukimwi wataweza kupika chakula chao kwa kipindi cha mwezi . Ni hali isiokubalika ” wanalaumu wakuu wa vijiji katika kambi ya Nyarugusu nchini Tanzania.
Watu hao kawaida wanapata msaada kutoka shirika la Danish Refugee Council, DRC. Shirika hilo liliwafahamisha kuwa hawako tena kwenye orodha ya HCR. Ni hatari iliyochukuliwa kinyume na wahusika.
” Ni kawaida HCR hatimaye imeingia katika mpango wa Tanzania wa kutulazimisha kurejea kwa nguvu. Kwanza kabisa, wajumbe wa shirika la DRC walituambia kwa kejeli kuwa tunaweza kwenda kupokea misaada yetu eneo la Mabanda ( nchini Burundi) . Kwa hiyo, sio kosa lililotokea katika data, badala yake, ni mpango uliondaliwa”, wanalaani wakimbizi.
Shirika la DRC lilikubali kuwasilisha tatizo hilo kwa HCR bila ahadi yoyote.
” Kwa nini tusipewe mkaa wakati katika ghala mkaa huo bado unapatikana na badaye wawasilishe tatizo hilo wakati wakifahamu kuwa hatuna chochote, na nguvu za kwenda kutafuta kuuni za kupikia nje ya kambi kama wengine ? Hiyo ni dalili kuwa ni mpango uliondaliwa. Hakika ni ukiukwaji mkubwa wa haki zetu wakati tuko katika kundi la watu ambao wanatakiwa kuwa katika uangalifu mkubwa wa mashirika ya misaada “, wanadai wakimbizi wa uraia wa Burundi wanaotembea na ulemavu.
Kitu na kinyume chake
Hata hivyo, upande wa wakimbizi wenye asili ya Kongo, orodha mpya zinaendelea kuandaliwa na kujumuisha watu wote bila ubaguzi kwa ajili ya kupewa misaada.
Nyarugusu inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi 110.000 wakiwemo zaidi ya elfu 50 wa uraia wa Burundi , wanaosalia wakiwa wakimbizi kutoka Kongo.