Cibitoke : waasi wa Rwanda wa kundi la FLN waripotiwa katika maeneo kadhaa ya umaa tarafani Mabayi, viongozi wachukuwa hatua ya kuwafungiana

Cibitoke : waasi wa Rwanda wa kundi la FLN waripotiwa katika maeneo kadhaa ya umaa tarafani Mabayi, viongozi wachukuwa hatua ya kuwafungiana

Hatua ya kufunga shughuli zote kwenye kituo cha Kivogero kinachotembelewa na waasi wanaozungumza Kinyarwanda waliopiga kambi katika msitu wa Kibira ilichukuliwa na mkuu wa tarafa ya Mabayi katika mkoa wa Cibitoke ( kaskazini magharibi mwa Burundi) .
Hatua hiyo ilipokelewa vibaya na wafanyabiashara. Mkuu wa tarafa hiyo alifahamisha kuwa alichukuwa hatua hiyo kwa ajili ya kulinda usalama. HABARI SOS Médias Burundi

Hatua hiyo ilichukuliwa mkuu wa tarafa ya Mabayi katika mkoa wa Cibitoke tangu wiki moja iliyopita.

Mahali yaliyolengwa ni pamoja na migahawa ya pombe na vyakula , maduka, pamoja na soko linalopatikana katika mlima wa Kivogero kwenye umbali wa kilometa mbili ya makao makuu ya tarafa hiyo.

Chanzo katika jeshi kinafahamisha kuwa waasi wa kundi la FLN wanaopigana dhidi ya serikali ya Kigali kutoka msitu wa Kibira siku ya ijumaa walihemea katika soko hilo.

” Wanaume hao wanaoficha sura zao na kuongea Kinyarwanda walipeleka bidhaa za vyakula kama unga wa mihogo, mahindi, maharagwe na viatu. Walirejea katika msitu huo kwenye mpaka na Rwanda ” chanzo chetu kilifahamisha.

Daima kulingana na chanzo hicho, kundi hilo linapata usaidizi kutoka Imbonerakure (wafuasi wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD) na kutoka kwa baadhi ya wanajeshi wa FDNB ( jeshi la Burundi) ambao wanawasaidia kupata usafiri wa bidhaa walizonunua.

Viongozi tawala wanasema kukasirikishwa na mwenendo huo wakati huu wa kufufuka kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya Gitega na Kigali”.

Wakaazi waliohojiwa wanaridhishwa na hatua hiyo ya mkuu wa tarafa na kuomba waasi hao wapigwe vita.

” Haikubaliki kuona watu hao wenye silaha wakijinufaisha na kutembea katika tarafa yetu kila mtu akiwaona bila kuguswa” alilaani mkaazi mmoja eneo hilo.

Shahidi huyo alihakikisha kuwa mbali ya waasi hao kupiga kambi ndani ya msitu wa Kibira kwa kipindi kirefu, wamekuwa wakionekana pia karibu na msitu huo mkubwa ndani ya tarafa za Mabayi na Bukinanyana.

Kamanda wa operesheni za kijeshi wa wakati huu ndani ya msitu wa Kibira alithibitisha habari hizo na kuzidi kuwa mashambulizi yanaandaliwa dhidi ya kundi hilo la silaha la watu wanaozungumza Kinyarwanda.

Machi iliyopita, katika mkutano kati ya gavana wa mkoa wa Cibitoke na mkoa wa magharibi mwa Rwanda, mkuu wa mkoa wa magharibi mwa Rwanda François Habitegeko aliwaomba viongozi wa Burundi kuwaambia wananchi waanze kuwafichuwa waasi wao wanaotoka nchini DRC katika mkoa wa Kivu ya kusini ambapo waasi wengi na makundi ya kigaidi yalipiga kambi na kupita katika tarafa za Mabayi na Bukinanyana hususan ili kurudi kuvuruga usalama kwenye ardhi ya Rwanda na kuwauwa wananchi wasiokuwa na hatia “.

” Ni budi kupeana habari na waasi waliokamatwa, wanatakiwa kuonyeshwa wananchi ili kulaani ushirikiano wao kabla ya kuhukumiwa kwa mjibu wa sheria” , alisisitiza bwana Habitegeko .

Previous Burundi : serikali iliamuru kusamehe ushuru kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kutoka nje ya nchi
Next Nyarugusu (Tanzania) : wakimbizi wawili kutoka Burundi wakufa kutokana na na maji ya mvua