Burundi : serikali iliamuru kusamehe ushuru kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kutoka nje ya nchi
Serikali ilichukuwa uamzi wa kusamehe ushuru kwa baadhi ya bidhaa mahitajio muhimu kama mchele, maharagwe, mbegu za mahindi, sukari ,…. kupitia tangazo la 30 machi 2023. Wizara ya fedha ilifahamisha kuwa bidhaa hizo za vyakula zilisamehewa ushuru wa hadi asilimia 1.5 ya ushuru wa forodhani. Hatua hiyo ilipokelewa vizuri na wafanyabiashara waliohojiwa. Hata hivyo wanahofia kuwa haitakuwa na athari kubwa kwenye soko. HABARI SOS Médias Burundi
Sheria hiyo ya kiwaziri ya tarehe 30 machi ilikuja kama suluhu kwa ajili ya kustawisha bei ya bidhaa hizo kwa mjibu wa wizara ya fedha.
Wafanyabiashara walipokea vizuri hatua hiyo. Kwa mjibu wao, bidhaa hizo sasa zinapatikana zaidi katika soko. Wanaomba serikali kuhakikisha hatua hiyo inachukuliwa kwa bidhaa zingine.
Lakini watumiaji upande wao wanasalia na wasi wasi. Hawaamini kuwa mabadiliko makubwa yatatokea.
Baadhi ya watalaam wa uchumi waliohojiwa upande wao wanadai kuwa hatua ya kusamehe ushuru wa baadhi ya bidhaa za vyakula inaweza kubadili hali lakini hapana hadi kupunguza bei kama inavyotarajiwa. ” Hatua hiyo itasaidia kuongeza kiwango cha bidhaa ndani ya nchi”, walizidi kusema baadhi.
Watalaam wa maswala ya uchumi wengine wanadai kuwa ni budi iwepo sera ya kitaifa ya kuongeza uzalishaji wa ndani ili bei ya bidhaa masokoni iweze kupunguka . Hata hivyo watalaam hao wanapendekeza ziwepo hatua za ziada ili hatua hiyo ya serikali iweze kuwa na athari inayodhihirika .