Kivu-kaskazini : MSF yatahadharisha kuhusu janga la kibinadamu kutokea eneo la mashariki mwa DRC kutokana na usalama mdogo
Janga la kibinadamu linaendelea kutokea katika mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC, lilitahadharisha shirika la MSF la waganga wasiokuwa na mipaka. Shirika hilo la waganga la kimataifa linatoa mwito kwa jamii ya kimataifa na viongozi wa Kongo kuongeza juhudi katika kukidhi mahitaji ya wananchi walioathiriwa na mapigano ya silaha. HABARI SOS Médias Burundi
Takriban watu milioni moja walikimbia mapigano baada ya kuibuka kwa kundi la silaha la M23 eneo la Kivu kaskazini katika kipindi cha mwaka ulioyopita. Misaada hadi sasa haitoshi kulingana na MSF.
Watu madhaifu wako katika hatari ya kuambukizwa maradhi yakiwemo maradhi ya kipindupindu, ukomaa , utapia mloo na kunyanyaswa kijinsia.
” Mzozo wa Kivu kaskazini umekuwa na madhara makubwa kutokana na ukubwa wake lakini pia misaada imekuwa ikichelewa katika maeneo mengi”, alifahamisha Avril Benoît, kiongozi mtendaji wa MSF-USA ambaye kwa sasa yuko mjini Goma.
” Kuna uhaba mkubwa wa misaada ili kukidhi mahitaji ya msingi ya wananchi kuhusiana na makaazi, madawa, vyakula na maji safi. Tunashuhudia kuwa madhara katika afya yao ni makubwa na yanaendelea kuongezeka, alizidi kusema.
Katika miezi ya hivi karibuni, ma mia ya ma elfu ya wananchi walitoroka makaazi yao na vijiji vyao na kwenda kuishi katika familia zilizowapokea na ndani ya vituo visivyokuwa rasmi. Pembeni ya Goma makaazi yaliyotengenezwa kwa kutumia hema za plastiki au vyandarua yamejaa huku watu wengine wakihifadhiwa ndani ya majengo ya kanisa na shule.
Wajumbe wa MSF wanahudumu katika vituo vya wakimbizi pembeni ya mji wa Goma tangu 2022 kwa kuwapa madawa bila kuwalipisha, gari za shirika hilo liliwapelekea maji safi na kuwajengea vyoo na baafu.
Mapigano yanaendelea kuripotiwa katika maeneo tofauti ya Kivu kaskazini na kuzidi kusababisha idadi kubwa ya wananchi kutimka
About author
You might also like
Makamba: walimu dhidi ya kulazimishwa kukusanya fedha na wakuu wa shule
Walimu hawa kutoka Kurugenzi ya Elimu ya Mkoa wa Makamba (kusini mwa Burundi) wanapinga kukusanywa kwa kiasi cha fedha kati ya faranga 4,000 hadi 14,000 za Burundi katika kurugenzi za
Kakuma (Kenya): zaidi ya wakimbizi 450 wa Sudan wanarejea kambini
Wakimbizi wa Sudan walikuwa wamekimbia mapigano kati ya jamii mbili za Sudan yaliyotokea Kalobeyei Julai mwaka jana. Wengi wao walikuwa wamepata hifadhi katika kambi ya Kakuma, wengine katika vijiji vinavyozunguka
Tanzania: UNHCR inajaribu kuwatuliza wakimbizi wa Burundi
Tume ya Juu ya Wakimbizi (UNHCR) inasema ina wasiwasi mkubwa na makala ya vyombo vya habari ambayo hivi karibuni yamesambazwa katika vyombo vya habari vya kitaifa na kimataifa kuhusu kulazimishwa