Nakivale-Mahama : zoezi la kuhesabu upya wakimbizi na kuhakiki tena hadhi zao za ukimbizi lasababisha wasi wasi kwa wahusika

Nakivale-Mahama : zoezi la kuhesabu upya wakimbizi na kuhakiki tena hadhi zao za ukimbizi lasababisha wasi wasi kwa wahusika

Katika kambi za wakimbizi za Nakivale nchini Uganda na Mahama nchini Rwanda wakati huu ni wa kuhesabu upya na kuhakiki hadhi za wakimbizi. Programu hiyo inatelezwa na HCR na inataraji kumalizika tarehe 23 aprili 2023 nchini Rwanda. Wahusika wanahofia hatua zinazoweza kuchukuliwa baada ya zoezi hilo. HABARI SOS Médias Burundi

Shughuli ya kukusanya takwimu mpya inafanyika katika kambi ambako wakimbizi walirejea makwao kwa hiari. Nchini Uganda, shughuli hiyo ilifanyika hususan katika kambi ya Nakivale na nchini Rwanda kambi ya Mahama ndio iliyolengwa.

” Ni zoezi la kuweka sawa mfumo wa kuorodhesha wakimbizi. HCR inafanya kazi hiyo ili kuimarisha mfumo huo na kuongeza uwajibikaji wake”, linaeleza tangazo la HCR kuhusu shughuli hiyo.

Wajumbe wa shirika hilo la umoja wa mataifa walifahamisha wakimbizi wa kambi ya Nakivale kuwa wanatakiwa kujiandaa kwa mabadiliko kuhusu namna wanavyopewa misaada baada ya zoezi hilo kumalizika.

” Mgawo wa chakula unaweza kupungua ikizingatiwa pia kuwa wakimbizi nao walipunguka kwa kiwango wa kutosha. Mfumo wa kuwasaidia kwa kuwapa pesa nao pia utashuhudia mabadiliko” walibaini.

Katika kambi ya wakimbizi ya Mahama, wakaazi wanasema pia kuwa wanajiandaa kupata baadhi ya habari mbaya. Lakini HCR inawatuliza.

” Munaweza kutaraji ucheleweshaji wa baadhi ya huduma, lakini hilo halitakuwa na madhara kwa programu ya misaada. Wanaopata msaada wa chakula na msaada mwingine hawataathiriwa na mchakato huo na wataendelea kupata misaada yao katika kipindi hicho kama kawaida”, HCR-Rwanda inatuliza na kuzidi kuwa mchakato wa kukusanya takwimu mpya utaendelea hadi 23 aprili 2023.

Wakimbizi wanataraji kuwa baada ya sensa hiyo, HCR badala yake itaongeza kuwango cha pesa ya matumizi inayotolewa ikizingatiwa kuwa bei zilipanda katika masoko ya ndani.

Nakivale inaorodhesha zaidi ya wakimbizi 140.000 wakiwemo elfu 33 kutoka Burundi wakati Mahama upande wake ikitoa hifadhi kwa wakimbizi elfu 45 idadi kubwa wakiwa kutoka Burundi.

Previous Cibitoke : mtu mmoja aliuwawa na mwingine kujeruhiwa katika msitu wa Kibira
Next Burundi : serikali iliamuru kusamehe ushuru kwa baadhi ya bidhaa za vyakula kutoka nje ya nchi