Cibitoke : mtu mmoja aliuwawa na mwingine kujeruhiwa katika msitu wa Kibira
Kundi la wachimba migodi wanaofanya kazi hiyo kwa kujificha walilengwa na wanajeshi usiku wa tarehe 8 kuamkia tarehe 9 aprili ndani ya msitu wa hifadhi wa Kibira. Tukio hilo lilijiri katika mlima wa Gafumbegeti, kijiji cha Butahana tarafa ya Mabayi katika mkoa wa Cibitoke (kaskazini magharibi mwa Burundi). Mtu mmoja aliuwawa na mwingine kujeruhiwa. HABARI SOS Médias Burundi
Muhanga ni mwenye umri wa miaka 40, mjumbe wa moja kati ya vyama vya ushirika 17 vinavyojihusisha na kuchimba madini tarafani Mabayi ambavyo havijapata leseni.
” kwa jumla ya vyama vya ushirika 21, ni nne peke ambavyo vina idhini ya kuchimba dhahabu, na muhanga alikuwa akifanya kazi hiyo kwa kujificha”, chanzo cha polisi kilieleza.
Mchimba madini mwingine anayefanya kazi kwa kujificha pia alijeruhiwa vikali baada ya kupigwa risasi tatu kwenye mguu wake wa kulia, kwa mjibu la chanzo cha polisi.
Angalau wachimba migodi 13 waliangamia wiki iliyopita kutokana na mvua kubwa iliyowakuta baadhi yao katika migodi miwili ya dhahabu ndani ya tarafa hiyo ya kaskazini magharibi mwa Burundi.
Tukio hilo liliibua hisia kwa wananchi ambao wanadai ni jukumu la viongozi tawala kujali maisha ya wachimba madini kwa kuwarahisishia kupata vifaa vya kujilinda pamoja na bima”.
Akihojiwa kuhusiana na mkasa huo, gavana wa mkoa wa Cibitoke anawataka wachimba madini wanaojumuika katika vyama vya ushirika kuwa na uvumilivu wakisubiri hatua ya kuruhusu uchimbaji madini kuanza kutekelezwa katika migodi tofauti.
Kiongozi huyo anaomba vikosi vya ulinzi na usalama kuendelea kuheshimisha hatua ya kuzuia uchimbaji wa dhahabu katika migodi kadhaa