Ituri: watoto waangamia katika mashambulizi ya makundi ya silaha mkoani Ituri

Ituri: watoto waangamia katika mashambulizi ya makundi ya silaha mkoani Ituri

Tangu disemba 2022, angalau watoto 60 waliuwawa katika vurugu za makundi ya silaha mkoani Ituri kaskazini mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo. Takwimu hizo zilitolewa na ujumbe wa shirika la umoja wa mataifa kwa ajili ya amani nchini Kongo (MONUSCO) ofisi ya mkoa. HABARI SOS Médias Burundi

Takwimu hizo za kusikitisha zilitolewa wakati wa uzinduzi wa mazungumzo ya jamii ya Hema yanayofanyika eneo la Bunia tangu siku chache zilizopita.

Karna Soro, mkuu wa MONUSCO mkoani Ituri, anaeleza kuwa watoto hao ni kati ya wananchi 310 waliouwawa na vikundi vinavyotajwa kuwa vibaya tangu mwishoni mwa mwaka jana mkoani Ituri.

” Kati ya tarehe mosi disemba 2022 na 21 machi 2023, tumeorodhesha watu 310 waliuwawa wakiwemo watoto 60. Nadhani katika lugha zetu za Afrika, hatuwezi kupata maneno ya kutumia ili kutoa maana ya hali hiyo. Ituri, Kongo ni ikulu yenu ya dhahabu. Licha ya matatizo na changamoto, tuungane. Damu ni nyingi, mateso ni mengi, hali hiyo inatakiwa kusimama”, alibaini.

Baadhi ya mashirika ya kutetea haki za watoto yanaomba ulinzi kwa watoto upewe kipau mbele na viongozi na pia makundi ya silaha.

Previous Ngozi : mfuasi wa chama cha CNL apatikana akiwa maiti
Next Cibitoke : mtu mmoja aliuwawa na mwingine kujeruhiwa katika msitu wa Kibira