DRC (Kalehe) : watoto saba wafariki dunia kwa kuteketezwa na moto ulioibuka katika kambi ya wahanga wa mafuriko

DRC (Kalehe) : watoto saba wafariki dunia kwa kuteketezwa na moto ulioibuka katika kambi ya wahanga wa mafuriko

Watoto saba wa angalau miaka mitano walifariki dunia katika ajali ya moto uliovamia kambi ya wakimbizi ya wahanga wa mafuriko ya mwezi mei iliyopita. Zaidi ya nyumba 400 ziliungua katika kambi ya Mushonezo eneo la Kalehe mkoa wa kivu kusini mashariki mwa DRC. HABARI SOS Médias Burundi

Nyumba zilizoteketea zilikuwa na paa la nyasi.

” Hatukuokoa kitu. Hakuna aliyefanikiwa kuokoa chochote kile ” alibaini Mushagalusa , mkimbizi wa Kalehe.

Amani alinusurika na mafuriko ya Nyamukubi mwezi mei uliopita. Alikuwa katika kambi mpya ya Mushonezo. Alipoteza kila kitu katika nyumba yake.

Thomas Bakenga mkuu wa wilaya ua Kalehe, alitangaza kuwa wahanga wote ni watoto wa chini ya miaka mitano.

Mkuu wa wilaya ya Kalehe anahakikisha kuwa serikali imo mbioni kujenga nyumba eneo la Lwako na Mushonezo kwa ajili ya kuwapa hifadhi waathiriwa na janga la Nyamukubi na Bushushu tarehe 4 mei iliyopita.

Takwimu zinazotolewa na serikali ya Kongo zinaonyesha kuwa katika mafuriko yaliyoathiri maeneo ya Nyamukubi na Bushushu katika wilaya ya Kalehe mwezi mei , watu zaidi ya 400 waliuwawa na wengine 5000 kupotea.

Previous Bururi : kiongozi wa gereza kuu ya Murembwe na wafanyakazi wenzake wawili wapewa adhabu ya kifungo cha miaka 7 na miezi 6 jela
Next Kesi-Bunyoni : sheria nchini Burundi yafunga akaunti za waziri mkuu wa zamani