Bururi : kiongozi wa gereza kuu ya Murembwe na wafanyakazi wenzake wawili wapewa adhabu ya kifungo cha miaka 7 na miezi 6 jela

Bururi : kiongozi wa gereza kuu ya Murembwe na wafanyakazi wenzake wawili wapewa adhabu ya kifungo cha miaka 7 na miezi 6 jela

Kanali wa polisi Patrice Nkurikiye kiongozi wa gereza kuu la Murembwe mkoani Rumonge (kusini magharibi mwa Burundi) na washirika wake wawili wahudumu katika idara ya sheria ndani ya gereza hilo, Florence Nimbona na Pélagie Nindamutsa wote walikatiwa kifungo cha miaka 7 na miezi 6 jela. Watatakiwa pia kulipa faini ya franka za Burundi milioni moja kila mmoja. Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya rufaa ya Bururi (kusini ) jumanne hii. Walipatikana na kosa la kuchangia katika ” kuvuruga usalama wa ndani ya nchi”. HABARI SOS Médias Burundi

Katika kesi ya mafumanio iliyofanyika wiki moja iliyopita, korti ya mkoa wa Bururi ilitoa hukumu kama hiyo ambayo iliendelezwa badaye na mahakama ya rufaa ya mkoa .

Watuhumiwa walipinga tuhuma zote dhidi yao. Tuhuma hizo zilihusu kuachiliwa huru kwa wafungwa waliokuwa wakifuatiliwa katika kesi ya mauwaji kwa kutumia mapanga. Mauwaji hayo yalitekelezwa kwenye makao makuu ya mkoa wa Bururi na viunga vyake katika mwezi mei iliyopita.

Siku moja baada ya kuwaachilia huru kwa muda wafungwa saba kati ya wale nane walikamatwa kwa mara nyingine.

Majaji watatu wa mahakama ya mkoa wa Bururi walikamatwa mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Majaji hao Antoine Ndendakumana, Léonard Nizigiyimana na Irène Mukeshimana wanazuiliwa katika gereza la Bururi. Wanafuatiliwa kwa kuwaachilia huru kwa muda wafungwa wanaohusishwa katika faili ya mauwaji kwa kutumia mapanga mkoani Bururi kwa mujibu wa mwendeshamashtaka wa jamuhuri.

Previous Mabayi : waziri mkuu wa serikali ya Burundi atishia kuwauwa watu wote wanaoshirikiana na waasi wa Rwanda waliopiga kambi ndani ya msitu wa Kibira
Next DRC (Kalehe) : watoto saba wafariki dunia kwa kuteketezwa na moto ulioibuka katika kambi ya wahanga wa mafuriko