Kesi-Bunyoni : sheria nchini Burundi yafunga akaunti za waziri mkuu wa zamani

Kesi-Bunyoni : sheria nchini Burundi yafunga akaunti za waziri mkuu wa zamani

Benki kuu ya Burundi BRB ( benki ya jamuhuri ya Burundi) ilitoa amri kwa mashirika ya fedha yote ili yasiruhusu kuondoa au kuweka pesa kwenye akaunti za waziri mkuu wa zamani Alain Guillaume Bunyoni. Benki kuu iliombwa na mahakama kuu kufanya hivyo. Kitita kilichofungwa bado kujulikana. HABARI SOS Médias Burundi

Mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri Léonidas Manirakiza alifahamisha kuwa hatua hiyo ilichukuliwa kwa lengo la kufuatilia vizuri kesi dhidi ya Bunyoni.

[….], Alain Guillaume Bunyoni ni kati ya watu wanaofuatiliwa kwa makosa mbali mbali”, yanasomeka katika tangazo lililosainiwa na mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri tarehe 14 agosti iliyopita.

Tarehe 22 agosti, Dieudonné Murengerantwari gavana wa benki kuu ya Burundi aliandikia barua ma benki ya mashirika mengine ya fedha na kuwaomba kutekeleza ombi la mwendeshamashtaka mkuu. Ombi hilo ni ” kutoruhusu zoezi lolote kwenye akaunti za Alain Guillaume Bunyoni, zinazoweza kuwa zimefunguliwa katika mashirika yenu ya fedha , hadi amri nyingine kutolewa”.

Vyanzo katika benki vinathibitisha kuwa walipata ma barua hayo mawili, moja ya mwendeshamashtaka na nyingine ya gavana wa benki kuu.

” akaunti zinazohusishwa na hatua hiyo ni zile za sarafu ya kigeni pamoja na sarafu ya ndani, walitoa ushahidi huo kiongozi wa shirika la fedha moja pamoja na mfanyakazi ndani ya moja kati ya benki za zamani nchini Burundi.

” Viongozi wanafamu sakata hilo na Bunyoni sio mtu wa kudanganywa kirahisi. Bila shaka alifungua akaunti zingine kwa majina ya watu wengine. Hatua itakayofuata ni kutafuta watu hao na kuchukuwa hatua kama hizo dhidi yao” alitoa tathmini hiyo mumiliki wa benki moja katika jiji la kibiashara la Bujumbura.

Hadi sasa kitita kilichofungwa kwenye akaunti hizo bado kujulikana. Lakini afisa huyo aliyetajwa katika faili nyingi za ubadilifu wa mali ya umma anatuhumiwa kumiliki makampuni mengi ya kuchimba madini mashariki mwa Kongo na bila shaka anamiliki utajiri mkubwa.

Alituhumiwa kwa kosa la kuvuruga usalama wa ndani na kuhujumu uchumi na kutumia ushawishi wake kwa ajili ya maaslahi yake binafsi na hivi karibuni liliongezwa shitaka la kumiliki silaha kinyume cha sheria na kumutukana rais. Muasi huyo wa zamani wa kihutu anaweza kukatiwa kifungo cha miaka 30 jela iwapo hatafaniwa kujitetea.

Familia yake na mawakili wake bado hawajajieleza kuhusu bhatua hiyo ya benki kuu ya Burundi.

Lakini wanaharakati wengi na waangalizi huru wanaona kuwa huo ni kulipiza kisasi na ni hali isioyokuwa na maslahi kwa warundi “.

Baada ya kukamatwa katika mazingira ya kutatanisha mwezi aprili iliyopita, waziri mkuuu wa zamani huyo alipelekwa katika gereza kuu ya Gitega ( mji mkuu wa kisiasa) mwezi julai iliyopita baada ya kumaliza zaidi ya miezi miwili akiwa katika gereza ya Ngozi ( kaskazini mwa Burundi). Korti kuu iliamuru aendelee kukaa jela.

Previous DRC (Kalehe) : watoto saba wafariki dunia kwa kuteketezwa na moto ulioibuka katika kambi ya wahanga wa mafuriko
Next Mebeba (Zambia) : HCR inakwenda kinyume na haki kuwazika wakimbizi