Mebeba (Zambia) : HCR inakwenda kinyume na haki kuwazika wakimbizi
Tangu muda mchache , HCR haotowi misaada kwa ajili ya mazishi kama ilivyokuwa kawaida. Wakimbizi wanaodai kuishi Katika mazingira magumu wanaomba shirika hilo la umoja wa mataifa kurejelea hatua hiyo. HABARI SOS Medias Burundi
Kisa cha hivi karibuni ni kile cha mkimbizi aliyefariki siku chache zilizopita. Familia ilimufanyia mazishi mjumbe wao katika mazingira magumu kutokana na uwezo mdogo.
” Mazishi ya Innocent mwenye asili ya mkoa wa Gitega ( kati kati mwa Burundi) yaliwagusa wote isipokuwa tu HCR. Raia huyo wa Burundi kwanza alikufa kwa sababu ya uzembe wa wauguzi katika kambi ya Meheba D Clinic. Harafu HCR haikufanya chochote ili kumuzika kwa heshma . Tulijipanga lakini hatuna uwezo wa kutosha, juhudi zetu hazikuweza kukidhi mahitaji ya mazishi ya heshma “, wanaeleza wakimbizi wa Burundi.
Na kulaaani : ” kawaida, HCR ingetakiwa kutuazima gari ya kusafirisha maiti, kutoa sandugu na kununua mashuka na blanketi, yaani vitu vya msingi. Lakini haikufanya chochote.
Huduma mbaya ya matibabu
Kwenye kituo cha afya kinasimamiwa na HCR eneo la Meheba ambalo kinakabiliwa na msongamano mkubwa, huduma za matibabu ni mbaya.
” Hakika, bora kliniki hiyo ifungwe sababu haitusaidii kitu. Kawaida ingetakiwa kuwa ya umma lakini inawapokea chini ya watu kumi wanaolazwa kwa miezi mitatu. Haileweki ! Mwishoni mwa wiki, wauguzi hawafanyi kazi, tunajiuliza iwapo na wagonjwa wanachukuwa likizo ! wakimbizi wa kambi ya Meheba wanasema.
Kwa mjibu wa vyanzo hivyo, kliniki hiyo pia inakosa madawa.
” ina na vidonge vya paracétamol hata waliojeruhiwa au mgonjwa anayesumbuliwa na matatizo yoyote anapewa kidonge hicho. Tulifahamu kuwa madawa yaliuzishwa “
Wakimbizi wana hasira dhidi ya HCR. Wanaomba shirika hilo la umoja wa mataifa na serikali ya Zambia kubadili mwenendo na kuhakikisha ulinzi wa wakimbizi katika nyanja zote.
Kambi ya Meheba ina zaidi ya wakimbizi elfu 27 wakiwemo warundi elfu tatu wenye asili ya Burundi