Kesi-Bunyoni : waziri mkuu wa zamani alihamishwa katika gereza ya waliofanya jaribio la mapinduzi
Waziri mkuu wa zamani Alain Guillaume Bonyoni kwa sasa ni mkaazi wa gereza kuu ya Gitega (mji mkuu wa kisiasa). Alihamishwa kutoka jela ya Ngozi (kaskazini mwa Burundi). Wakati huo huo, kamanda wa zamani wa kikosi cha kutuliza fujo kanali wa polisi Désiré Uwamahoro ambaye angechangia chumba na muajiri wake wa zamani atabaki gerezani. Chumba cha ushahuri cha mahakama kilitoa uamzi huo jumanne hii alasiri. HABARI SOS Médias Burundi
Ni majira ya saa tisa na nusu ambapo waziri mkuu wa zamani Alain Guillaume Bunyoni aliwasili katika gereza ya Gitega kwa mujibu wa mashahidi.
” Alikuja na gari aina ya pick-up ambayo ilijaa askali polisi wenye silaha kubwa . Gari nyingine aina ya pick-up ilikuwa ikilinda usalama wa gari ya kwanza. Na hiyo ilikuwa na askali polisi waliokuwa na silaha nzito ” shahidi mmoja alishuhudia.
Masaa machache kabla ya ujio wa mgeni huyo ndani ya gereza la mji mkuu wa kisiasa, eneo maluum kwa ajili ya kumpokea lilikaguliwa kwa mara ya mwisho.
” Viongozi wakuu wa polisi na idara ya ujasusi waliwasili eneo hilo. Nenda rudi zilipunguzwa ” vyanzo katika gereza hilo la Gitega vilihakikisha.
Kwa mujibu wa vyanzo katika idara ya waliotoa ushuhuda kwa sharti la kubana majina yao kwa sababu hawana ruhsa ya kuongea na wandishi wa habari, kamanda wa zamani wa kikosi cha kutuliza fujo kanali wa polisi Désiré Uwamahoro angetakiwa kupelekwa katika chumba kimoja na bosi wake wa zamani. Anazuiliwa Gitega.
Ujenzi wa eneo hilo ulianza mwanzoni mwa mwezi mei wakati wanaume hao wawili walipopelekwa jela.
Ni vyumba viwili vyenye ukubwa wa mita 4×4 kila kimoja na ukuta wa sentimeta 50 pamoja na bafu na choo vya ndani. Ni maafisa wa taasisi ya serikali ya upango miji makaazi na ujenzi (OBUHA) waliofanya ujenzi huo chini ya uangalizi wa brigedia wa polisi Emmanuel Ndayiziga mkuu wa itifaki wa SNR ( idara ya ujasusi) . Mbele ya vyumba hivyo viwili, kuna uwanja wa mazoezi wa ukubwa wa mita 8×6. Vyumba hivyo pamoja na uwanja vilijengwa na theluji na kupewa nguzo imara.
” Chumba cha pili kwa sasa kinakaliwa na askali polisi wenye jukumu la kumuzuia kutoroka Bunyoni” chanzo katika idara ya magereza kiliambia SOS Médias Burundi.
Wiki iliyopita, vyombo vya sheria vya Burundi vilifahamisha kuwa vinaendelea kutafuta ushahidi mpya kuhusu mashtaka dhidi ya Bunyoni.
Alifuatiliwa kwa kuharibu usalama wa ndani, kuhujumu uchumi wa nchi na kutumia madaraka kwa maslahi yake binafsi pamoja na kumiliki silaha kinyume cha sheria na kumutukana rais, waziri mkuu huyo wa zamani anaweza kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela.
Jela kuu ya Gitega ambako Bunyoni anazuiliwa, inawahifadhi pia waliofanya mapinduzi na wapinzani wengi waliofanya mandamano dhidi ya muhula mwingine wa rais Nkurunziza ulioleta utata katika mwaka wa 2015.
Mwishoni mwa mwaka uliopita, shirika la Human Right Watch liliwaomba viongozi wa Burundi kuhakikisha haki katika kesi hiyo na kuruhusu waangalizi wa kimataifa kufuatilia ili haki za Bunyoni ziweze kuheshimiwa “.
Muasi huyo wa zamani wa kihutu chini ya vikwazo vya marekani alifutwa katika wadhifa wake na rais Ndayishimiye mwanzoni mwa mwezi septemba 2022 katika mazingira ya giza .