Burundi – Rwanda : mke wa rais wa Burundi afanya ziara katika nchi jirani ambayo hadi sasa mumeo apata tabu kutembelea

Burundi – Rwanda : mke wa rais wa Burundi afanya ziara katika nchi jirani ambayo hadi sasa mumeo apata tabu kutembelea

Nchi ya Rwanda inapokea tangu jumatatu kongamano la sita la kimataifa la ” Women Deliver ” kuhusu usawa wa kijinsia. Mmoja kati ya wageni maluum ni mke wa rais wa Burundi, nchi zamani adui. HABARI SOS Médias Burundi

Kongamano la kimataifa linalozungumzia afya ya akinama, haki na ustaawi wa wasichana na akinamama linafanyika tangu jumatatu ndani ya mji mkuu wa Kigali.

Zaidi ya watetezi wa usawa wa kijinsia elfu 6 wanahudhuria kongamano hilo. Mmoja kati ya wageni wa heshma ni marais kama rais wa Sénégal, Ethiopia na rais wa Hangari pamoja na wake wa ma rais wa nchi mbali mbali kama Burundi , nchi zamani aduwi wa nchi hiyo inayohifadhi kongamano hilo.

Angeline Ndayishimiye alipitia katika mpaka wa ardhini wa Gasenyi-Nemba ( Kaskazini) .

Alilakiwa na mshahuri wa kwanza katika ofisi ya mke wa rais wa Rwanda na badaye kupokelewa rasmi na mke wa rais wa Rwanda Jeannette Kagame mjini Kigali.

” Kuona wake hao wawili wa ma rais wa nchi zamani madui wakipeana zawadi , ni mabadiliko makubwa katika historia ya nchi hizo mbili. Lakini haieleweki pia kuona ni mke wa rais wa Burundi aliyeanza kufanya hatua hiyo kubwa mbele kabla ya mumeo ambaye amechagua kutuma ujumbe mwingi mjini Kigali kabla yake”, ametoa tathimini hiyo raia mmoja wa Burundi mjini Kigali kabla ya kutumai kuwa ” desturi ya ujumbe wa chuki na vita kati ya nchi hizo mbili zilizobadilika hautatolewa tena”.

Mwezi februari 2023, rais wa Rwanda Paul Kagame alitembelea mwenzake wa Burundi ndani ya mji mkuu wa Bujumbura ( mji wa kiuchumi) wakati wa kikao cha 20 cha wakuu wa nchi za EAC kuhusu mzozo mashariki mwa RDC.

” Kigali inasubiri ziara ya kurudishia “.

Nchi hizo mbili ziliamuru kufanya ujirani mwema tangu 2020, wakati Gitega ikiendelea kutuhumu ndugu yake wa Kaskazini kuwapa hifadhi waliofanya jaribio la mapinduzi la mei 2015.

Iwapo Kigali haijawafichua ” madui hao ambao wanatafutwa kwa udi na uvumba na sheria ya Burundi, kengele itasikika hivi karibuni ikizingatiwa ziara hiyo ya viongozi wakuu wa nchi hizo mbili”.

Waziri wa diplomasia wa Burundi hivi karibuni alifahamisha kuwa ” Kigali haitashindilia kwa muda mrefu juu ya kukataa ombi hilo ambalo si faida hata kidogo kwake”.

Previous Kesi-Bunyoni : waziri mkuu wa zamani alihamishwa katika gereza ya waliofanya jaribio la mapinduzi
Next Nyarugusu (Tanzania) : maiti ya mwanamke mmoja yapatikana ndani ya shamba