Nyarugusu (Tanzania) : maiti ya mwanamke mmoja yapatikana ndani ya shamba
Ni muili wa mwanamke ambaye hakutambulika. Ulipatikana kwenye mstari wa kutenganisha eneo linalokaliwa na raia wa Kongo na lile wa raia wenye asili ya Burundi. Uchunguzi tayari imeanza ili kutambua aliyefariki. HABARI SOS Médias Burundi
Muili huo ni wa mwanamke wa kati ya miaka 25 na 30, kwa mujibu wa mashahidi. Muili huo uligunduliwa na wapita njia mapema jumatano hii asubuhi.
” Maiti ilikuwa imeanza kuharibika na kutoa harufu mbaya ambayo ilisababisha wapita njia kuangalia. Waliita mara moja polisi ambao walikuja kuchukuwa maiti hiyo. Polisi hiyo iliahidi pia kufanya uchunguzi kwa ajili ya kumutambua muhanga” , walisema wakimbizi.
Muili uliwekwa kwenye chumba cha kuhifadhi maiti katika kijiji cha 3 eneo la raia wenye asili ya Kongo ili kusubiri kipindi cha siku tatu kwa ajili ya kijaribu kutambua muhanga kabla ya mazishi yake yanayotarajiwa wekendi ijayo, kwa mujibu wa viongozi wa kijamii.
Viongozi hao waliitisha mikutano ndani ya kila kijiji ili kuangalia iwapo kuma mtu ambaye atadai kutafuta mtu wake.
Taarifa za kwanza za polisi na viongozi tawala zinasema huenda muhanga ” alinyongwa ” sababu muili wake ulikuwa na majeraha.
Hadi sasa, jina la muhanga, na uraia wake bado kujulikana ikizingatiwa kuwa kambi ya Nyarugusu inawapa hifadhi raia kutoka Burundi pamoja na Kongo wanaokadiriwa kuwa wakimbizi laki moja na elfu 10.