Burundi : ni budi kuwa makini katika kuwatuma wasichana nchini Saudi Arabia, alisema mke wa rais

Burundi : ni budi kuwa makini katika kuwatuma wasichana nchini Saudi Arabia, alisema mke wa rais

Mke wa rais wa Burundi analaani kuona wasichana wadogo wakiacha shule na kutoroka maeneo yao ya asili na kwenda kutafuta ajira katika nchi za warabu. Angeline Ndayishimiye alitoa wito kwa mashirika yanayohusika na kutafuta ajira kwa ajili ya wasichana hao kuhakikisha mazingira mazuri yanakuwepo katika mchakato wote wa kuwatuma wasichana hao katika nchi hizo. Ni tamko alilofanya kwenye mpaka wa Gasenyi-Nemba wakati akirejea kutoka kongamano la kimataifa la ” Women deliver awamu ya 2023″ lililozinduliwa mjini Kigali jumatatu tarehe 17 julai. HABARI SOS Médias Burundi

Mke wa rais alifahamisha kuwa hakuna anayeweza kuzungumzia haki za akimama bila kujali haki za wasichana wadogo.

Alirejelea swala la akinamama na wasichana waliotumwa nchini Saudi Arabia kufanya kazi za ndani.

” Niliguswa na vidéo ya akidada hao waliokuwa wakiomba msaada siku chache zilizopita. Niliwaona wakilala chini wakiwa watano. Ni kwa sababu hiyo ninawaambia wadau wanaowatuma wasichana hao kuwa waangalifu kabla ya kuwatuma huko” alisisitiza na sauti kubwa Angeline Ndayishimiye.

Kwa mtazamo wake, wazazi pia wanatakiwa kuwa makini na kuwakataza watoto wao kutoroka shule kwa ajili ya kwenda kutafuta pesa. ” Iwapo wasichana hao wote wanakwenda kutafuta ajira na kuacha shule shule, mstakabali wa nchi utakuwa aje ? Tunahitaji wanawake waliosoma, wenye akili kwa ajili ya kuendeleza nchi” alizidi kusema.

Na kumalizia : ” Mimi, kama mama ninawaomba wahusika wote kufanya uchunguzi ili kufahamu vizuri yanayowasubiri upande wa pili. Tutetee haki zao na kuwajibike kabla hatujachelewa “.

Mwishoni mwa wiki iliyopita , Inès Sonia Niyubahwe msemaji wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa alikanusha mabaya yanayowafikia wasichana hao ambayo waliyatangaza kupitia video, na kuhakikisha kuwa ubalozi wa Burundi ulituma ujumbe katika maeneo ya kupokea wasichana hao na ujumbe huo ulisema kuwa hakuna tatizo.”

Ines Sonia Niyubahwe alitoa wito kwa wasichana hao waliotumwa kufanya kazi katika nchi za warabuni ” kusalia watulivu na kusubiri maeneo yao ya kazi katika siku chache zijazo”.

Zoezi la kwanza la kuwatuma rasmi nchini Saudi Arabia wanawake hao na wasichana wanaotafuta ajira lilifanyika tarehe 19 mei 2023. Kwa jumla zaidi ya wasichana 800 hadi sasa walitumwa chini ya mwamvuli wa mkataba kati ya Burundi na Saudi Arabia kama alivyofahamisha msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni.

Previous Nyarugusu (Tanzania) : maiti ya mwanamke mmoja yapatikana ndani ya shamba
Next Tanzania : biashara haramu ya watoto wa kike ambao ni wakimbizi kutoka Burundi kambini