Tanzania : biashara haramu ya watoto wa kike ambao ni wakimbizi kutoka Burundi kambini
Inashuhudia ” biashara ya wasichana wadogo” katika kambi za wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania. Wanaolengwa zaidi ni wasichana wenye umri chini ya miaka 18. Wanaelekea hasa katika miji ya Mwanza, Arusha na Dar es Salaam. Polisi iliingilia kati. Uchunguzi unasubiriwa lakini matokeo yake yakizidi kuchelewa. SOS Médias Burundi ilipokea ushuhuda wa kusisimua.
Chantal*, ni jina la kuazima. Ni mshichana ambaye hivi karibuni ataadhimisha kumbukumbu ya miaka 17. Anaishi katika eneo la 5 (kijiji chake na namba ya nyumba vumebanwa kwa ajili ya usalama).
Wakati nilipokwenda, nilikuwa nikikaribia miaka 15, nilirejea mwaka mmoja na nusu badaye. Waliniahidi kazi ya mshahara na nikaacha masomo. Wazazi wangu hawakujuwa mahali nilipokuwa”. alieleza kwa sharti la kubana jina lake. Anakumbuka mahala alipokwenda. ” Ni Mwanza”, anajibu.
Anazidi kuwa alivunjika moyo baada ya kushuhudia kuwa kazi ambayo aliahidiwa sio ile ambayo alilazimika kufanya.
” Nilitakiwa kuwa mfanyakazi wa ndani na kulea watoto. Lakini badala ya kazi hiyo, nilinyanyaswa kijinsia. Nilikuwa nikilazimika kulala na wanaume wawili hadi watatu kwa siku moja. Mwanamke aliyenipokea na kunipa hifadhi, alikuwa akinipatia kati ya shilingi elfu 3 na 4 za Tanzania kwa ajili ya kununua pampasi wakati nikifahamu kuwa mwanaume mmoja aliweza kulipa kati ya shilingi 20 na 30 za kitanzania ( kati ya dola 8 na 12) hata na zaidi, wakati akijihisi kuridhika na huduma “, alitoa ushahidi huo msichana huyo, machozi yakitiririka.
Biashara hiyo haramu ambayo iliwagusa wasichana zaidi ya mia moja katika kambi za Nduta na Nyarugusu iliandaliwa vizuri. Chanzo cha uhakika kinafahamisha kuwa mtandao wa akinamama wa Burundi hufanya kazi kwa ushirikiano na kundi jingine la wanawake wa Tanzania.
” Kundi hilo la akinamama ndani ya kambi linajihusisha na kuangalia pamoja na kuchagua wasichana ambao wanaona kuwa ni wazuri na maumbile ya kawaida. Kundi hilo linawadanganya na kuwaahidi kazi ya mshahahara. Mazungumzo yote yanafanyika kwa siri na wasichana hao hutoka nje ya kambi bila kuwaambia wazazi. Badaye, kundi la ndani ya kambi hulipa nauli na wasichana hao wanapelekwa katika vituo vya mjini “, alifahamisha kiongozi wa kijamii ambaye alijaribu kufichua biashara hiyo bila mafanikio.
Miji ya mafikio kwa sehemu kubwa ni Mwanza kwenye mwambao wa ziwa Victoria kaskazini mwa nchi, Arusha kaskazini mashariki mwa Tanzania na Dar es Salaam, mji mkuu wa kiuchumi wa nchi.
” Wasichana hao wanapokelewa na kundi jingine la akinamama wa Tanzania wanaokodesha nyumba ili kutumia watoto hao katika maovu. Akinamama hao hutafuta wanaume ambao watalala na wasichana hao kwa sharti la kulipa pesa”, vyanzo vyetu vinaeleza.
” Mimi nilikuwa ninaishi na wasichana wengine watano. Sijuwi walitoka wapi. Ni badaye ambapo nilijuwa kuwa sisi wote ni wakimbizi waliotoka katika kambi za wakimbizi “, alifahamisha Chantal* ambaye akirejea katika usawa kama anavyosema.
Wakati Chantal* alipokosekana katika kambi ya Nduta, familia yake ilimutafuta mahala pote. Familia ilitoa malalamiko kwa polisi ambayo upande wake ilifanya uchunguzi bila mafanikio. Wakati aliporejea msichana huyo, familia yake ilitoa taarifa kwa polisi na kutoa habari zote kuhusiana na hali hiyo.
Majibu ya polisi yalikuwa ya kushangaza kwa mujibu wa familia yake.
” Walitushahuri kwenda kuomba ushahuri nasaha kwa mwanasayikoloji na kufanya vipimo vya afya ili kumulinda na virusi na maradhi mengine ambayo anaweza kuwa alipata wakati wa majanga. Hakuna hata neno moja kuhusu uchunguzi au kuwafuatilia watu wanaotuhumiwa. Kwa hiyo inamaanisha kuwa polisi ilihusika “, wazazi wa Chantal* walifahamisha.
Kwa mjibu wa viongozi eneo hilo, kuna uwezekano polisi ikahusika.
” Tulijaribu kufuatilia nenda rudi na kufichua watu wanaotuhumiwa kujumuika katika mtandao huo. Kwa mara kadhaa polisi ilifanya uchunguzi na kukwama kwenye hatua fulani. Mtandao huo unawapa hongo askali polisi wanaojaribu kufuatilia faili hiyo. Badaye ni sisi ambao walioanza kupata vitisho na uoga wa kuendelea “, alitoa ushahidi mkuu wa zamani wa kijiji cha Nduta.
Mabaya yanayowakabili wasichana hao wahanga wa ” biashara haramu ya watu ndani ya kambi”, hayawezi kuelezeka.
” Maradhi mengi ukiwemo ukimwi, maradhi ya sehemu za siri, mimba zisizotarajiwa, vifo, vitisho,….” orodha ya ndefu.
Anafahamisha kuwa alipata msaada kutoka kwa mchungaji wa kanisa mmoja la Mwanza ambaye alimulipia nauli ya kurudi kambini.
” Nilitolewa nje ya moto. Lakini kuna wasichana wanaoishia kufurahia hali hiyo sababu wanapata chakula, kunywaji na shilingi kwa ajili ya vipodozi wakati hapa ndani ya kambi wakiwa hawana chochote”, alieleza kabla ya kulaani biashara hiyo na kufahamisha kuwa wasichana hao wanahitaji kuokolewa.
” Ninaweza kutoa ushuhuda mbele ya taasisib zinazohusika, lakini ninahofia usalama wangu” alimalizia akiwa na majonzi.
Idadi ya waathiriwa wa biashara hiyo ya watu ni vigumu kujulikana lakini vyanzo ndani ya kambi vinadai kuwa wanakadiriwa kuwa zaidi ya mia moja , na kuzidi kuwa zoezi hilo lilianza kwa uficho miaka miwili iliyopita.
Tanzania inawapa hifadhi wakimbizi kutoka Burundi zaidi ya 126.600