Burundi : nchi imepata mwendeshamashtaka mkuu mpya
Ni Léonard Manirakiza, ameidhinishwa jumanne hii na baraza la seneti. Wanaharakati wanasema kuwa hawataraji mambo makubwa kutoka kwake lakini wameamuru kujizuia kueleza chochote. HABARI SOS Médias Burundi
Léonard Manirakiza ameidhinishwa na wajumbe wa baraza la seneti 38 kwa jumla ya 39. Ni waziri wa sheria aliyeeleza kuhusu wasifu wake. Domine Banyankimbona amesema ni mtu shujaa bila kueleza sababu zilizopelekea baraza kuu ya wanasheria kuondoa uaminifu kwa mwendeshamashtaka mkuu wa zamani Sylvestre Nyandwi.
Bwana Manirakiza hadi jumanne hii alikuwa mfanyakazi katika korti kuu kama mkuu wa kitengo. Kabla ya wadhifa huo, alihudumu kama mwendeshamashtaka wa jamuhuri katika mkoa wake wa asili wa Muramvya ( kati kati) . Kati ya mwezi juni na agosti 2016, aliwafunga watoto 6 waliotuhumiwa kuharibu picha ya hayati Pierre Nkurunziza ndani ya kitabu. Mkoani Gitega ( mji mkuu wa kisiasa) alishughulikia faili ya mauwaji ya Ndadaye ambayo zaidi ni kesi ya kisiasa kuliko kuwa ya kisheria kwa mujibu wa watu waliopewa adhabu ya kifungo cha hadi maisha jela, waliokuwepo au wale ambao hawakuwepo katika kesi hiyo dhidi ya mauwaji ya Melchior Ndadaye, rais wa kwanza wa Kabila la wahutu aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka wa 1993.
[…], anafahamika kwa sifa ya kutovumilia wengine. Hayo yalidhihirika wakati alipotoa amri ya kuwafunga wafuasi wa chama cha MSD ( chama kwa ajili ya ushirikiano na demokrasia) na watoto walioharibu picha ya hayati Pierre Nkurunziza ndani ya kitabu cha wanafunzi ” ,ameeleza Anschaire Nikoyagize kiongozi wa shirika la Iteka, shirika la zamani kabisa la kutetea haki za binadamu nchini Burundi.
Upande wake wakili Dieudonné Bashirahishize, ” mwendeshamashtaka wa jamuhuri mpya wakati wa safari yake ya kikazi hajaonekana kama mtetezi wa uhuru wa sheria lakini bado ana nafasi ya kutenda na kuchangia katika kuboresha mfumo wa sheria nchini Burundi”.
” Kwa vile alishiriki mwenyewe katika kesi za kisiasa ambazo zinaendeshwa na maslahi ya kisiasa, ataweza kupata uaminifu iwapo ataanza kwa kusimamisha hatua hizo ambazo zinaatoa uaminifu kwa sheria ya Burundi. Jukumu hili mpya ni gumu, tutawahukumu kwa kazi watakayofanya. Atakubali kutumiwa au atakuwa na ushujaa wa kukataa ? historia itatuonyesha ” alimalizia mwanaharaka hiyo ambaye kwa sasa yuko ukimbizini.
Gérard Ngendabanka katibu wa kudumu wa baraza kuu la majaji alifahamisha kuwa majaji wengine 8 waliodhinishwa ili kufanyia kazi katika korti kuu, watasaidia kumaliza wingi wa faili ndani ya korti hiyo wakati majaji wakiwa idadi isioyotosha”.
Léonard Manirakiza ni kabila la wahutu mwenye asili ya mkoa wa Muramvya. Atachukuwa nafasi ya Sylvestre Nyandwi, wa Kabila la wahutu pia mzaliwa wa mkoa wa Bujumbura ( magharibi) ambaye alikuwa kwenye wadhifa huo tangu agosti 2016.