Nyiragongo : hali ya kibinadamu kwenye kituo cha wakimbizi cha adventiste Kasenyi inatisha

Nyiragongo : hali ya kibinadamu kwenye kituo cha wakimbizi cha adventiste Kasenyi inatisha

Wakimbizi hao wa ndani hawapokei msaada wowote. Ni hali inayozidisha udhaifu wao na hivyo kuwasukuma katika mitaa kuomba omba. Ni tahadhari ya mkuu wa kituo cha adventiste Kasenyi ambaye anazidi kuwa hali yao ya kibinadamu ni mbaya. Viongozi wa kituo hicho wanaomba misaada. Kituo hicho kunapatikana karibu ya mji wa Goma makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mujibu wa Jean-Claude Nguriye, miezi mingi imemalizika wakimbizi hao wa ndani wakiwa hawana msaada wowote.

Wanalazimika kuingia katika mitaa ili kuomba misaada na hivyo kujiweka katika hatari ya kukumbwa na matatizo mengi zikiwemo ajari za barabarani, mateso na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya akinamama na wasichana wadogo.

” Tuko hapa tangu tarehe 27 oktoba 2022. Hatujapewa msaada wowote. Tunaishi maisha mabaya . Tunaomba omba ili tuweze kupata cha kutafuna. Watu wa roho nzuri wanatupatia chakula lakini wengine wanatutesa. Wakimbizi wengine wanapata ajari za barabarani na wanawake wanabakwa. Wale waliokosa chakula, wanarudi nyuma na kulala tumbo ikiwa haina kitu”, anaeleza mkuu wa kituo hicho.

Ili kujiepusha na mabaya zaidi, kiongozi wa kituo cha adventiste cha Kasenyi anaomba misaada kutoka kwa mashariki ya kiutu na serikali na kurejea kwa amani ndani ya eneo hilo.

Kituo cha wakimbizi cha adventiste Kasenyi tayari kiliorodhesa vifo vya watu wanne kutokana na njaa pamoja na matatizo mengine kama uhaba wa maji na kujaa kwa vyoo.

Zaidi ya watu 100000 walitoroka makaazi yao na ma kumi ya wengine kuuwawa katika mashambulizi ya vikundi vya silaha ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo ( DRC) kwa mjibu wa ripoti ya shirika la umoja wa mataifa UN mwanzoni mwa mwezi machi.

Previous Burundi : nchi imepata mwendeshamashtaka mkuu mpya
Next Kirundo : mvulana mmoja alifariki dunia baada ya kupigwa na Imbonerakure