Kirundo : mvulana mmoja alifariki dunia baada ya kupigwa na Imbonerakure

Kirundo : mvulana mmoja alifariki dunia baada ya kupigwa na Imbonerakure

Ezéchiel Ntahinduka, miaka 14 alifariki jumatatu tarehe 24 julai akiwa kwenye hospitali ya mkoa. Kwa mjibu wa mashahidi, kijana huyo wa kiume alifariki kutokana na kipigo aliyefanyiwa na Jean Marie Nkurunziza mjumbe wa tawi la vijana wa chama tawala (CNDD-FDD). Kisa hicho kilitokea kwenye mlima wa Nyakibingo tarafani Ntega mkoa wa Kirundo Kaskazini mwa Burundi. Wazazi wake wanaomba muhusika akamatwe na adhibiwe kwa uhalifu wake. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa mashahidi, mtoto huyo alipigwa. Alituhumiwa kupanda nyuma ya gari iliyokuwa inatembea.

” Jean Marie Nkurunziza, Imbonerakure, alimupiga vikali kijana huyo wa miaka 14. Ilikuwa tarehe 15 julai mwaka huu. Mtoto alipigwa vikali kama nyoka. Kwa bahati mbaya hakupata msaada”, anakumbuka mzee wa miaka zaidi ya 60 ambaye analaani kuona watu wote walisikia uoga wa kuingilia kati ili kuokoa mtoto huyo.” Tumezoea uhalifu unaofanywa na Imbonerakure hao hapa kwetu tarafani Ntega”, anaendelea kusema mzee huyo.

Habari zinazosambaa zinasema kuwa afya ya mtoto huyo ikiendelea kuwa mbaya tangu alipokabiliwa na unyanyasaji huo. Familia ilimpeleka kwenye kituo cha afya cha Rushubije kwa ajili ya matibabu lakini hali yake ilikuwa mbaya zaidi.

Jumamosi asubuhi, familia ya mtoto ilimpeleka kwenye hospitali ya Kirundo. Lakini kijana huyo alifariki dunia siku hiyo hiyo.

Chanzo katika utawala kinahakikisha kuwa Jean Marie Nkurunziza tayari alitoroka.

” Viongozi tawala wa china huenda walimficha ili asikamatwe na polisi “, alifahamisha mteule mmoja katika kijiji. Kwa mjibu wa chanzo hicho watu wengine watatu wamehusishwa katika faili hiyo. Wawili wanazuiliwa katika jela ya Ntaga.

Familia ya mtoto inaomba sheria ichukuwe mkondo wake.

Previous Nyiragongo : hali ya kibinadamu kwenye kituo cha wakimbizi cha adventiste Kasenyi inatisha
Next Nduta (Tanzania) : uhaba mkubwa wa damu wakati wa mripuko wa malaria