Uvira : zaidi ya watu wengine 300 kutoka Burundi wakimbilia nchini DRC

Wanapewa hifadhi katika kambi ya muda ya Sange ndani ya wilaya ya Uvira mkoa wa kivu-kusini (mashariki mwa DRC) tangu siku chache zilizopita. Wahusika ni kutoka hususan katika mikoa ya Cibitoke na Bubanza (kaskazini magharibi mwa Burundi). HABARI SOS Médias Burundi

Warundi hao wanadai kuwa walifukuzwa ndani ya ardhi zao na serikali.

” Serikali yetu ilitunyanganya ardhi zetu. Hakuna haki ya kwenda katika mashamba yetu. Kilichosalia kwetu ni kukimbia” walilaani wajumbe wa kundi kundi hilo waliozungumza na SOS Médias Burundi.

Ardhi hizo zinazozungumziwa zinapatikana eneo la Mabayi, Nyarure, Rugombo, Mbazamiduha katika mkoa wa Cibitoke pamoja na Kibira-Rukoko mkoani Bubanza.

Mmoja kati ya viongozi wa kambi hiyo ya muda ya Sange anafahamisha kuwa takriban waomba hifadhi hao wote, wanakutania katika hoja moja : Kunyanganywa ardhi zao”.

Kuhusu swala hilo, gavana wa mkoa wa Cibitoke anapinga madai hayo. Carême Bizoza anafahamisha kuwa serikali ilirejesha ardhi ambazo zilikuwa miliki yake. Anatoa mifano ya ardhi za Nyarure na Mbazamiguha.

Mkoani Bubanza, gavana anasema ni eneo ambako kunafanyika mazoezi ya kijeshi.

Lakini waomba hifadhi hao kutoka Burundi ” wanadai ni ukiukwaji wa haki zao”.

Katika miaka ya hivi karibuni, walishuhudiwa warundi wanaokimbilia nchini RDC kutokana na njaa mbali na wale waliokimbia kutokana na unyanyasaji dhidi ya wapinzani lakini hii imekuwa mara ya kwanza kwa nchi hiyo kubwa ya Afrika ya kati kuwapokea watu wenye asili ya Burundi kwa idadi kubwa wanaotoroka kwa sababu ya Kunyanganywa ardhi za kilimo.

Previous Tanzania : viongozi tawala wawahamasisha wakimbizi kuhusu kuheshimu sheria ambazo wao wanazikiuka kila mara
Next Kivu-kaskazini : MSF yatahadharisha kuhusu janga la kibinadamu kutokea eneo la mashariki mwa DRC kutokana na usalama mdogo

You might also like

Siasa

Mutwana: Kutengwa na shinikizo kwenye kando ya uchaguzi wa wakuu wa vilima

SOS Médias Burundi, Rutana, Julai 4, 2025 – Wakati uchaguzi wa madiwani wa kilele cha mlima unapokaribia kwenye kilima cha Mutwana, kilicho katika eneo la Butezi la tarafa ya Giharo,

Siasa

Bubanza: wakazi walazimika kukaribisha mwenge wa amani, shule na biashara kufungwa

Biashara, shule, utawala, wakazi… Kila mtu alilazimika kwenda kuukaribisha mwenge wa amani Jumanne hii katika wilaya ya Bubanza. Iko katika jimbo la Bubanza (magharibi mwa Burundi). Msafara huo uliozinduliwa na

Siasa

RTNB: Kutoka huduma ya umma hadi kinara wa matangazo ya CNDD-FDD

SOS Médias Burundi Bujumbura, Septemba 10, 2026 — Shirika la Taifa la Utangazaji la Burundi (RTNB)—ambalo linafadhiliwa na fedha za umma na kimsingi linapaswa kuwahudumia raia wote—linazidi kushutumiwa kwa kufanya