Masisi: mapigano makali kati ya kikosi cha Burundi na kundi la M23
Mapigano makali ya kundi la M23 dhidi ya wanajeshi wa Burundi wa kikosi cha jumuiya ya Afrika mashariki yalifanyika siku ya ijumaa. Jeshi la Kongo linahakikisha kuwa zaidi ya wapiganaji 10 wa kundi la M23 waliuwawa na wengine kukamatwa. HABARI SOS Médias Burundi
Ni mchana wa ijumaa ambapo mapigano hayo yaliibuka. Yalifanyika eneo la Jérusalem katika kitongoji cha Malehe katika wilaya ya Masisi. Msemaji wa kikosi cha kikanda cha EAC alifahamisha katika tangazo siku ya ijumamosi kuwa mapigano yaliendelea hadi usiku na jumamosi asubuhi.
” Mapigano yaliibuka wakati wapiganaji wa M23 walitaka kudhibiti tena baadhi ya ngome walizoacha wiki kadhaa zilizopita. Wanajeshi wa Burundi wajumbe wa kikosi cha kikanda wanaohudumu eneo hilo, walipinga hilo”, yanaeleza mashirika ya kiraia eneo hilo.
Habari hizo zimethibitishwa na jeshi la Kongo katika mkoa wa Kivu kaskazini. Jeshi hilo linahakikisha kuwa angalau wapiganaji 10 waliuwawa, wengine walikamatwa pamoja na zana za kijeshi.
” Tunapongeza ushujaa wa wanajeshi wa Burundi walifungua moto kwa ajili ya kuwalinda wananchi dhidi ya uvamizi wa M23. Wananchi wanahitaji amani” , alibaini luteni kanali Guillaume Ndjike Kaiko msemaji wa gavana mwanajeshi wa mkoa wa Kivu kaskazini.
Mashirika ya kiraia ya ndani yanaripoti kuwa yaliona gari za kubeba wagonjwa sikifanya nenda rudi kwa ajili ya kuchukuwa maiti na majeruhi waliokuwa wamevalia sare za kijeshi , wengine nguo za kawaida ambao idadi yao na uraia bado kujulikana.
Hii ni mara ya kwanza kwa wanajeshi wa kikosi cha EAC kilichotumwa nchini DRC kupigana dhidi ya M23.
Upande wake, kundi la M23 halijasema chochote kuhusu mapigano hayo ya waasi wake dhidi ya wanajeshi wa Burundi.
Kulingana na makubaliano ya Luanda ( Angola) na Nairobi (Kenya) , kundi la M23 liliahidi kuacha ngome zake za zamani na kuzikabidhi kikosi cha EAC tangu disemba 2022.
Lakini katika baadhi ya maeneo, vyanzo vyetu vinasema kuwa kuna uvunjaji wa amri hiyo ya kusitisha vita inayoendelea. Burundi ina kikosi vitatu vilivyotumwa kwenye ardhi ya nchi hiyo kubwa jirani wa magharibi. Walitumwa katika mkoa wa Kivu ya kusini na Kivu kaskazini katika jukwa la ushirikiano kati ya mataifa hayo mawili na chini ya mwamvuli wa jumuiya ya Afrika mashariki.
You might also like
DRC: Corneille Nangaa na wasaidizi wake walioidhinishwa na Marekani
Katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa Alhamisi hii, Marekani ilitangaza kuwa imechukua vikwazo dhidi ya Corneille Nangaa, mkuu wa Muungano wa Mto Congo (AFC) na baadhi ya washirika wake.
Cibitoke: wanajeshi sita wasimamishwa baada ya kupurukushana na Imbonerakure
Wanajeshi hao sita walikuwa wakifanyia kazi kwenye kituo cha Ruhagarika . Ni katika tarafa ya Buganda ndani ya mkoa wa Cibitoke kaskazini magharibi mwa Burundi karibu na mto wa Rusizi
Uvira: Wanajeshi 17 wa Burundi wauawa katika mapigano huko Rugezi
SOS Media Burundi Takriban wanajeshi 17 wa Burundi wanaopigana pamoja na FARDC waliuawa wakati wa mapigano makali dhidi ya waasi huko Twirwaneho, katika eneo la Fizi katika jimbo la Kivu
