Malawi: zaidi ya wakimbizi 400 kutoka nchi za maziwa makuu wakamatwa na polisi

Malawi: zaidi ya wakimbizi 400 kutoka nchi za maziwa makuu wakamatwa na polisi

Ma mia ya wakimbizi kutoka Rwanda, Burundi na Kongo ambao kati yao kuna waliokuwa wakifanya biashara kinyume cha sheria walikamatwa katika mji wa Lilongwe na miji mingine baada ya kupinga amri ya kurudi ndani ya kambi ya wakimbizi ya Dzaleka, kambi peke ambayo inapatikana katika nchi hiyo ya kusini mashariki mwa Afrika. HABARI SOS Médias Burundi

Waziri wa usalama wa ndani alitangaza kupitia radio na televisheni ya taifa kuwa zaidi ya wakimbizi 400 pamoja na waomba hifadhi wakiwemo watoto walikamatwa katika operesheni ya polisi iliyozinduliwa wiki mbili zilizopita katika kata nyingi za mji mkuu Lilongwe.

Kamata kamata hiyo imejiri miezi miwili baada ya ilani ya mwisho kutolewa na serikali kwa wakimbizi kurudi katika kambi iliyojaa watu ya Dzaleka, kwenye umbali wa kilometa takriban arbaini kutoka Lilongwe.

” Muda uliotolewa ulimalizika. Tulieleza kuwa iwapo watu hao hawatajipeleka, polisi itaingilia kati kuwalazimisha kufanya hivyo”, alifahamisha msemaji wa wizara hiyo.

Idadi kubwa ya wakimbizi na waomba hifadhi nchini Malawi ni wenye asili ya nchi za jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo (DRC), inayokabiliwa na mzozo na uhalifu pamoja na Rwanda na Burundi.

Baadhi ya wajumbe wa jamii ya warundi mjini Lilongwe wanasema kushangaa kwa sababu, serikali hiyo iliahidi kulinda wakimbizi.

” Kamata kamata hiyo ni aina ya ukiukwaji mkubwa wa wazi wa haki za kimataifa za wakimbizi na husababisha mazingira ya hofu na hali ya sintofahami kwa wahusika. Harafu wakimbizi kutoka kambini hawaruhusiwi kufanya tena biashara yao hapa, wananyanganywa na polisi au wananchi mali zao zote. Wananchi hao wanakasirikisha na biashara zetu”, walifahamisha hayo wakimbizi kutoka kambi ya Dzaleka waliozungumza na SOS Médias Burundi.

Hayo ni wakati ambapo tangu mwanzoni mwa mwezi huu, wakimbizi waliokuwa wakiishi katika miji ya Malawi wakiwa walianza kurejea katika kambi ya Dzaleka, wakiwa na nia ya kuheshimu ilani iliyotolewa na serikali ili waondoke katika miji. Athari ni kwamba kambi imezidiwa na idadi kubwa.

Wakimbizi wanafahamisha kuwa wako katika mgogoro na wajasiliamali wa nchi hiyo ambao wamekuwa wakiwatishia kwa kipindi kirefu kuwafukuza wakimbizi katika maeneo ya masoko sababu wakimbizi hao huwaletea ushindani usiokuwa sahihi katika maswala ya bei.

Kambi ya Dzaleka inawapa hifadhi waomba hifadhi kutoka Burundi , jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, Ethiopia, Rwanda na Somalia.

Kambi hiyo ilitaraji kuwapokea wakimbizi takriban elfu kumi lakini kwa sasa kuna zaidi ya elfu 50. Wakimbizi waliokuwa wakiishi katika miji hukadiriwa kuwa nusu ya wale waliokuwa wakiishi kambini.

Shirika la HCR linaomba viongozi wa Malawi kusimamisha hatua hiyo kwa ajili ya kuepusha msongamano katika kambi hiyo ambayo tayari imezidiwa na idadi kubwa ya watu mara tano zaidi ya uwezo wake.

Shirika hilo la umoja wa mataifa linalohusika na wakimbizi linadai kuwa idadi kubwa ya watoto watakuwa katika hatari ya kuacha shule huku wafanyabiashara wengi waliokuwa wakijihudumia wakilazimika kurejea ndani ya kambi ambapo watategemea tu misaada.

Nchi ya Malawi iliwapokea wakimbizi karibu ya elfu 70 pamoja na waomba hifadhi kwa mjibu wa HCR.

Previous Burundi: utawala wa rais Ndayishimiye unafanya mauwaji kama ule wa mtangulizi wake Nkurunziza
Next Burundi : Maadhimisho ya siku ya kitaifa ya shujaa wa uzalendo bila ujumbe rasmi