Burundi : Maadhimisho ya siku ya kitaifa ya shujaa wa uzalendo bila ujumbe rasmi

Burundi : Maadhimisho ya siku ya kitaifa ya shujaa wa uzalendo bila ujumbe rasmi

Alhamisi hii, Burundi iliadhimisha kwa mara ya tatu siku ya kitaifa ya uzalendo ambayo pia ni kwa niaba ya rais Nkurunziza aliyepandishwa na kupewa hadhi ya mfano na shujaa wa uzalendo katika mwaka wa 2021. Hakuna ujumbe rasmi kuhusiana na siku hiyo, rais Ndayishimiye alikuwa ziarani kuhudhuria mkutano wa 22 wa wakuu wa nchi na ma rais wanachama wa jumuiya ya soko la pamoja katika nchi za Afrika ya mashariki na kusini ambapo aliteuliwa kuwa naibu kiongozi. Watetezi wa haki za binadamu nchini Burundi wanasema ” rais Nkurunziza aliacha urithi wa kutatanisha”. HABARI SOS Médias Burundi

Siku hiyo ilitangazwa kama siku ya mapumziko. Imekuwa siku kuu nyingine ya ziada katika nchi hiyo ndogo ya Afrika mashariki.

Sherehe kuhusiana na siku kuu ya kitaifa ya uzalendo pamoja na maadhimisho ya tatu ya kifo cha rais Pierre Nkurunziza zilifanyika mkoani Gitega. Walioshiriki katika sherehe hizo, ni wale waliopata mualiko peke. Hakuna wananchi wa kawaida walioshiriki kama inavyokuwa katika siku kuu zingine. Hakuna ujumbe rasmi mbali na kutangaza wasifu wa hayati Nkurunziza. Wasifu huo ulitolewa na mmoja kati ya washahuru katika ofisi ya rais Ndayishimiye. Rais huyo aliamuru kumusifu mtangulizi wale kupitia ukurasa wake wa Twitter, ” ni rais mmoja peke alieyewaachia warundi nchi iliyostawi” .

Akinama na wanaume waliozunguza na wandishi wetu ndani ya mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura, wanakumbuka kuwa ni mtu aliyeanzisha kutoa huduma pasina kulipa kwa akinamama wanaojifungua na watoto kusoma bila kulipa ada ya shule.

” Angekuwepo, hatungeshuhudia ughali huu wa gharama za maisha na mdororo huu wa bei. Angeyamaliza haya ” wakaazi wengi wa mjini wamesisitiza .

Urithi wenye kutatanisha

Lakini wakaazi wengine wamemtaja rais huyo wa zamani wa Burundi kama ” katili ambaye visa vyake vibaya viliacha madhara mabaya kwa nchi yake”.

Kwa mjibu wa Janvier Bigirimana kiongozi wa harakati maarufu Tournons la Page-Burundi, tubadili ukurasa-Burundi, ” urithi wa rais Nkurunziza ni wa kutatanisha”.

” Angekuwa hai, angetakiwa kuwajibishwa mbele ya sheria kutokana na maovu mengi yaliyotendeka chini ya utawala wake. Kumuenzi kama shujaa wa uzalendo ni matusi kwa wahanga wa utawala wake,” alieleza mwanaharaki huyo.

Maoni ni kama hayo pia kwa wakimbizi wa Burundi katika kambi ya Nduta nchini Tanzania.

” Ni kutokana na ubinafsi wake ambapo tulijikita katika matatizo haya. Kupenda kwake utawala kulipelekea nchi katika janga. Tarehe 8 juni ingekuwa siku ya kukumbuka watu wetu waliouwawa ” , walieleza wakimbizi waliozungumza na SOS Médias Burundi. Wakimbizi hao wanamaliza miaka nane ukimbizini kutokana na muhula wa kutatanisha wa hayati Nkurunziza.

Pierre Nkurunziza aliuwawa kutokana roho yake iliyosimama tarehe 8 juni 2020 baada ya miaka 15 ya utawala wake kulingana wa viongozi wa Burundi.

Previous Malawi: zaidi ya wakimbizi 400 kutoka nchi za maziwa makuu wakamatwa na polisi
Next Burundi : noti mpya za elfu tano na elfu kumi zawekwa katika mzunguko wa pesa