Kivu-kaskazini : MSF yatahadharisha kuhusu janga la kibinadamu kutokea eneo la mashariki mwa DRC kutokana na usalama mdogo
Janga la kibinadamu linaendelea kutokea katika mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC, lilitahadharisha shirika la MSF la waganga wasiokuwa na mipaka. Shirika hilo la waganga la kimataifa linatoa mwito kwa jamii ya kimataifa na viongozi wa Kongo kuongeza juhudi katika kukidhi mahitaji ya wananchi walioathiriwa na mapigano ya silaha. HABARI SOS Médias Burundi
Takriban watu milioni moja walikimbia mapigano baada ya kuibuka kwa kundi la silaha la M23 eneo la Kivu kaskazini katika kipindi cha mwaka ulioyopita. Misaada hadi sasa haitoshi kulingana na MSF.
Watu madhaifu wako katika hatari ya kuambukizwa maradhi yakiwemo maradhi ya kipindupindu, ukomaa , utapia mloo na kunyanyaswa kijinsia.
” Mzozo wa Kivu kaskazini umekuwa na madhara makubwa kutokana na ukubwa wake lakini pia misaada imekuwa ikichelewa katika maeneo mengi”, alifahamisha Avril Benoît, kiongozi mtendaji wa MSF-USA ambaye kwa sasa yuko mjini Goma.
” Kuna uhaba mkubwa wa misaada ili kukidhi mahitaji ya msingi ya wananchi kuhusiana na makaazi, madawa, vyakula na maji safi. Tunashuhudia kuwa madhara katika afya yao ni makubwa na yanaendelea kuongezeka, alizidi kusema.
Katika miezi ya hivi karibuni, ma mia ya ma elfu ya wananchi walitoroka makaazi yao na vijiji vyao na kwenda kuishi katika familia zilizowapokea na ndani ya vituo visivyokuwa rasmi. Pembeni ya Goma makaazi yaliyotengenezwa kwa kutumia hema za plastiki au vyandarua yamejaa huku watu wengine wakihifadhiwa ndani ya majengo ya kanisa na shule.
Wajumbe wa MSF wanahudumu katika vituo vya wakimbizi pembeni ya mji wa Goma tangu 2022 kwa kuwapa madawa bila kuwalipisha, gari za shirika hilo liliwapelekea maji safi na kuwajengea vyoo na baafu.
Mapigano yanaendelea kuripotiwa katika maeneo tofauti ya Kivu kaskazini na kuzidi kusababisha idadi kubwa ya wananchi kutimka
You might also like
Nduta (Tanzania): mkimbizi wa Burundi aliyeuawa
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka thelathini alikutwa amekufa, nje ya kambi hiyo, mkoani Tanga, kaskazini-mashariki mwa Tanzania ambako alikuwa akifanya shughuli zake za useremala. Familia yake inataka uchunguzi ufanyike.
Bujumbura: ufisadi wa kingono huwasukuma watoto wengi kutumia njia tofauti za uzazi wa mpango
Watoto wengi katika mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura mara kwa mara hutumia njia za uzazi wa mpango, hasa “kidonge cha asubuhi baada ya”. Maduka ya dawa 15 katika jiji
Bujumbura Inakabiliwa na mgogoro wa vyoo vya umma: Wakazi washutumu faini inayoonekana si ya haki
SOS Médias Burundi Bujumbura, Novemba 12, 2025 – Hatua mpya ya serikali imezua hasira miongoni mwa wakazi wa mji mkuu wa kiuchumi. Tangu kuchapishwa kwa agizo la pamoja la Mawaziri
