Kivu-Kaskazini : zaidi ya wananchi 200 waliuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja eneo la Beni
Katika kitongoji cha Ruwenzori wilaya ya Beni mkoa wa Kivu-kaskazini (mashariki mwa DRC) , zaidi ya watu 200 waliuwawa katika kipindi cha mwezi mmoja. Takwimu hizo zinatolewa na ofisi ya uratibu wa mashirika ya kiraia ya Kongo. Idadi kubwa ya wahanga waliuwawa kwa mapanga na kundi la ADF (nguvu zilizoungana kwa ajili ya demokrasia). HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mjibu wa Jade Vutsapu, muhudumu katika ofisi ya uratibu wa mashirika ya kiraia nchini Kongo, tangu usiku wa tarehe 9 machi hadi 09 aprili, ” waasi wa ADF waliwauwa watu 200 katika wilaya moja ya Beni huku kitongoji cha Bashi kikiorodhesha idadi kubwa “.
” Katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia usiku wa tarehe 8 kuamkia tarehe 09 aprili , tulihesabu zaidi ya watu 200 waliouwawa kwa mapanga na waasi wa ADF. Idadi kubwa waliuwawa katika kitongoji cha Bashu, ambapo idadi iliyoorodheshwa ni zaidi ya vifo 38 waliouwawa eneo la Mukondi na 8 walikufa eneo Mwasa katika kipindi cha siku moja, lakini pia eneo la Kirindera usiku wa tarehe 11 kuamkia 12 machi watu 20 waliuwawa. Eneo la Masabanda kuelekea Oicha waliuwawa watu 21 na kuna maeneo mengine ambapo mauwaji hayo yalifanyika. Tunakasirika kuona mauwaji hayo yakitekelezwa katika maeneo ambako kuna idadi kubwa ya wanajeshi “, alibaini mwanaharakati huyo.
Jade Vutsapu anatumai kuwa mauwaji hayo yanatekelezwa katika mpango wa mauwaji ya halaiki yanayolenga wananchi wa wilaya ya Beni.
Anaomba serikali kutathimini upya mkakati wake wa amani na usalama katika eneo hilo.
You might also like
Goma: karibu vifo thelathini na zaidi ya watu 3,800 walioathiriwa na janga la tumbili huko Kivu Kaskazini.
Takriban visa 3,843 vya Mpox vimerekodiwa katika mkoa wa Kivu Kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Hayo yamesemwa na mkuu wa kitengo cha afya cha mkoa wa Kivu
Ituri: Raia 27 wauawa na 11 hawajulikani walipo katika mashambulizi mapya yanayohusishwa na kundi la ADF
SOS Médias Burundi Mambasa, Julai 26, 2026 — Angalau raia 27 wameuawa na wengine 11 hawajulikani walipo kufuatia mfululizo wa mashambulizi mapya yanayohusishwa na kundi la Allied Democratic Forces (ADF)
Kivu-kaskazini : watetezi wa haki za binadamu wako hatarini katika maeneo ya migogoro ya silaha
Watetezi wa haki za binadamu katika wilaya ya Rutshuru wanatahadharisha kuhusu vitisho dhidi yao kutoka kwa viongozi wa makundi ya waasi. Wanatoa takwimu za wanaharakati 18 waliouwawa na makundi ya
