Rutana-Giharo : viongozi wa chama tawala walazimisha wapinzani kutoa michango kwa ajili ya siku kuu yao

Rutana-Giharo : viongozi wa chama tawala walazimisha wapinzani kutoa michango kwa ajili ya siku kuu yao

Kulingana na mkuu wa chama cha CNL tarafani Giharo mkoa wa Rutana (kusini mashariki mwa Burundi), viongozi wa eneo hilo wa chama tawala walitoa mamlaka kwa Imbonerakure ( wajumbe wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD) ya kukusanya kwa nguvu vyakula na pesa kwa lengo ya kuandaa sherehe iliyopangwa kufanyika tarehe 22 aprili 2023. Viongozi wa chama cha upinzani cha CNL wanaomba viongozi tawala kuwalinda dhidi ya vitisho na kuwanyamanzisha. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa viongozi wa chama cha upinzani cha CNL, Imbonerakure hao wanafanya mikutano kwa ajili ya kupanga zoezi la kukusanya vyakula hususan katika kijiji cha Giharo.

” Kwa zaidi ya wiki moja Ernest Niyonizeye kiongozi wa Imbonerakure katika kijiji cha Giharo hutembea maeneo yote ya kijiji hicho kutoa vitisho kwa wananchi na kutahadharisha yoyote ambaye atapinga zoezi hilo la ukusanyaji muhimu kwa ajili ya siku kuu yao” alifahamisha kiongozi wa chama cha CNL.

Vitu vinavyokusanywa ni vyakula ambavyo kwa sehemu kubwa ni mbegu za mahindi, na franka 4000 kwa kila mtu, wakisema ni kwa ajili ya kununua nguo za vijana wafuasi wa chama tawala kwa ajili ya siku kuu hiyo.

” Mazoezi ya kijeshi kwa ajili ya kuwatishia wale waliopinga nia yao yalianza tangu tarehe 7 aprili kuanzia saa kumi na mbili jioni” wanasikitika wafuasi wa chama cha upinzani.

Mbali ya zoezi hilo la ukusanyaji, Imbonerakure hao kwa ushirikiano na ma katibu wa vijiji wa chama tawala, husambaza vitisho kwa lengo la kuwalazimisha wafuasi wa chama cha CNL kujiunga na chama cha CNDD-FDD kwa ajili ya kuepuka na matatizo, viongozi wa chama cha CNL wanalalamika.

Viongozi hao wa chama kikuu cha upinzani tarafani Giharo wanamutuhumu Alexis Baraguma katibu wa chama cha CNDD-FDD katika kijiji cha Giharo, Ernest Niyonizeye mkuu wa Imbonerakure pamoja na katibu wa chama hicho katika maeneo ya mlima wa Bayaga Frédéric Nyamweru kuwa chanzo cha kufanya michango hiyo kwa nguvu.

Wanaomba viongozi tawala kuwalinda wafuasi wa vyama vya upinzani wanaotishiwa kifo na Imbonerakure hao ambao wanazidi kutoa ujumbe kuwa ” ambao watapinga mpango wao, watauwawa”.

Jumapili hii, kiongozi mkuu wa chama cha CNL alikosoa ” ujumbe wa chuki unaotolewa na katibu mkuu wa chama cha CNDD-FDD na hali ya kutovumiliana kisiasa inayoendelea kushuhudiwa nchini Burundi”. Ilikuwa katika kongamano la wafuasi wa chama chake katika mji mkuu wa kisiasa wa Gitega.

Miaka iliyopita, viongozi kimkoa wa chama tawala walijulikana sana kwa kukusanya michango kwa nguvu au kujipa kwa nguvu kwa ajili ya mandalizi ya matukio ya chama chao yanayojilikana au la kwa ngazi ya kitaifa.

Previous DRC-Goma : serikali ya Kongo haijakuwa tayari kuzungumza na kundi la M23
Next Kakuma (Kenya) : maradhi ya usafi mdogo yatishia waomba hifadhi

You might also like

Utawala

Burundi : viongozi wa Burundi wapiga marufuku kongamano la kimataifa la akinamama waumini wa kikristu

Viongozi wa Burundi alhamisi hii walifahamisha kuwa kongamano la kimataifa la kikristu la akinamama halitafanyika. Kongamano hilo liliandaliwa na shirika linaloongozwa na mchungaji kutoka Rwanda. Waziri wa mambo ya ndani

Siasa

Uchaguzi wa Rumonge: Vitisho, Kutengwa kwa Wawakilishi, na Udanganyifu Mkubwa vimechafua mchakato wa Upigaji Kura.

SOS Médias Burundi Rumonge, Juni 5, 2025 – Burundi ilipofanya uchaguzi wake wa wabunge na manispaa Alhamisi hii, jimbo la kusini-magharibi la Rumonge lilikuwa na dosari kubwa. Kati ya vitisho

Usalama

Rumonge: Migogoro ya ndani ya CNDD-FDD kabla ya uchaguzi wa vilima

SOS Médias Burundi Rumonge, Agosti 22, 2025 – Huku uchaguzi wa milimani ukipangwa kufanyika Jumatatu, Agosti 25, kitongoji cha Kanyenkoko katika mji wa Rumonge, katika Mkoa wa Burunga (kusini mwa