Burundi : ni budi kuwa makini katika kuwatuma wasichana nchini Saudi Arabia, alisema mke wa rais
Mke wa rais wa Burundi analaani kuona wasichana wadogo wakiacha shule na kutoroka maeneo yao ya asili na kwenda kutafuta ajira katika nchi za warabu. Angeline Ndayishimiye alitoa wito kwa mashirika yanayohusika na kutafuta ajira kwa ajili ya wasichana hao kuhakikisha mazingira mazuri yanakuwepo katika mchakato wote wa kuwatuma wasichana hao katika nchi hizo. Ni tamko alilofanya kwenye mpaka wa Gasenyi-Nemba wakati akirejea kutoka kongamano la kimataifa la ” Women deliver awamu ya 2023″ lililozinduliwa mjini Kigali jumatatu tarehe 17 julai. HABARI SOS Médias Burundi
Mke wa rais alifahamisha kuwa hakuna anayeweza kuzungumzia haki za akimama bila kujali haki za wasichana wadogo.
Alirejelea swala la akinamama na wasichana waliotumwa nchini Saudi Arabia kufanya kazi za ndani.
” Niliguswa na vidéo ya akidada hao waliokuwa wakiomba msaada siku chache zilizopita. Niliwaona wakilala chini wakiwa watano. Ni kwa sababu hiyo ninawaambia wadau wanaowatuma wasichana hao kuwa waangalifu kabla ya kuwatuma huko” alisisitiza na sauti kubwa Angeline Ndayishimiye.
Kwa mtazamo wake, wazazi pia wanatakiwa kuwa makini na kuwakataza watoto wao kutoroka shule kwa ajili ya kwenda kutafuta pesa. ” Iwapo wasichana hao wote wanakwenda kutafuta ajira na kuacha shule shule, mstakabali wa nchi utakuwa aje ? Tunahitaji wanawake waliosoma, wenye akili kwa ajili ya kuendeleza nchi” alizidi kusema.
Na kumalizia : ” Mimi, kama mama ninawaomba wahusika wote kufanya uchunguzi ili kufahamu vizuri yanayowasubiri upande wa pili. Tutetee haki zao na kuwajibike kabla hatujachelewa “.
Mwishoni mwa wiki iliyopita , Inès Sonia Niyubahwe msemaji wa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa alikanusha mabaya yanayowafikia wasichana hao ambayo waliyatangaza kupitia video, na kuhakikisha kuwa ubalozi wa Burundi ulituma ujumbe katika maeneo ya kupokea wasichana hao na ujumbe huo ulisema kuwa hakuna tatizo.”
Ines Sonia Niyubahwe alitoa wito kwa wasichana hao waliotumwa kufanya kazi katika nchi za warabuni ” kusalia watulivu na kusubiri maeneo yao ya kazi katika siku chache zijazo”.
Zoezi la kwanza la kuwatuma rasmi nchini Saudi Arabia wanawake hao na wasichana wanaotafuta ajira lilifanyika tarehe 19 mei 2023. Kwa jumla zaidi ya wasichana 800 hadi sasa walitumwa chini ya mwamvuli wa mkataba kati ya Burundi na Saudi Arabia kama alivyofahamisha msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni.
You might also like
Kuzuiliwa kwa mwandishi wa habari Sandra Muhoza – Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa wanahabari wa SOS Médias Burundi
Tunalaani vikali kuzuiliwa kiholela kwa mwenzetu, Sandra Muhoza, aliyefungwa tangu Aprili 18 mjini Bujumbura. Ukandamizaji huu wa makusudi dhidi ya vyombo huru vya habari ni dharau kwa uhuru wa kujieleza
Burundi: Mahakama ya Rufaa ya Mukaza yatangaza mamlaka yake yameisha – Sandra Muhoza aendelea kuzuiliwa licha ya kumalizika kwa hatia
SOS Médias Burundi Bujumbura, Julai 1, 2025 — SOS Media Burundi imefahamu kwamba Mahakama ya Rufaa ya Mukaza, iliyoko katika jiji la kibiashara la Bujumbura, ilitoa uamuzi wake Juni 13,
Gitega : hakuna sheria miaka 27 baada ya mauwaji ya askofu Joachim Ruhuna
Askofu Joachim Ruhuna mkuu zamani wa dayosezi ya Gitega aliuwawa tarehe 9 septemba 1996. Mauwaji hayo yalifanyika karibu na mto wa Mubarazi. Katika kipindi hicho, maeneo ya Bugendana na Mutaho
