Goma: kijana mdogo uuwawa na askali polisi katika kituo cha kuandika wapiga kura

Goma: kijana mdogo uuwawa na askali polisi katika kituo cha kuandika wapiga kura

Dieudonné Bagenda, miaka 20 aliuwawa kwa kupigwa risasi. Risasi lilimpata kichwani akiwa katika kituo cha kuorodhesha wapiga kura cha Byahi alhamisi hii katika kata ya Bujovu ndani ya mji wa Goma makao makuu ya mkoa wa Kivu kaskazini. Kulingana na ushahuda ulipatikana eneo hilo, chanzo cha mgogoro ni kitita cha pesa walichokubaliana kati ya muhanga na askali polisi anayelinda kituo hicho. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa ushuhuda, makubaliano ni kwamba Dieudonné Bagenda angetakiwa kumpa pesa askali polisi huyo baada ya kujiorodhesha. Baada ya kukosa kadi yake, muhanga alikataa kuheshimu makubaliano na yote yakaanzia hapo.

” Walikubaliana kuwa baada ya kupewa kadi, kijana huyo angemupa franka 5000 sarafu za Kongo askali polisi huyo. Baada ya kujichakaza, kijana alijikuta hana pesa hiyo waliokubaliana, hali ambayo haikumufurahisha polisi huyo. Aliamuru kumpiga risasi kichwani “, alieleza shahidi mmoja kwa hasira.

Mtu mwingine alifahamisha kuwa muhanga hakupata kadi yake ya mpiga kura, na alikuwa akifuatilia mchakato wote kupitia dirisha.

” Alikuwa bado hajapata kadi yake. Iwapo angemufuatilia baada ya kupata kadi yake, hapo tungeelewa lakini alikuwa alifuatilia kupitia dirisha. Kuliko kumuambia aondoke, askali polisi huyo alimufuatilia hadi ndani ya kata na kumumalizia maisha”, alitoa ushuhuda mkaazi wa Goma machozi yakitiririka.

Muili wa muhanga ulibaki kwa dakika chache katika kituo cha kuorodhesha wapiga kura wakisubiri wananchi waliokuwa na hasira watulie.

Badaye muili ulipelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti kwa kusubiri matokeo ya uchunguzi.

Kituo hicho cha kuorodhesha wapiga kura kilivamiwa na kusambuliwa na vijana kabla ya polisi kuwasili eneo la tukio.

Hivi karibuni, askali polisi mwingine aliwasha moto ndani ya kituo cha kuandikisha wapiga kura kaskazini mwa mji wa Goma bila hata hivo kusababisha hasara.

Mashirika ya kiraia yanaomba viongozi wa usalama kuwaelekeza askali polisi wanaohudumu kwenye vituo vya kuandikisha wapiga kura.

Previous Gatumba : mafuriko yalazimisha familia nyingi kukimbia
Next Bujumbura : wakaazi wasumbuka kupata maji safi