Bujumbura : wakaazi wasumbuka kupata maji safi

Bujumbura : wakaazi wasumbuka kupata maji safi

Maji safi yamekuwa adimu katika kata za kaskazini na kusini mwa jiji kuu la kiuchumi. Katika baadhi ya kata, wakaazi wanaweza kumaliza wiki moja bila kupata huduma hiyo. Wananchi wanahofia kuambukizwa maradhi yanayosababishwa na uchavu hususan wakikumbuka katika akili za karibu lilivyokuwa janga la kipindupindu. HABARI SOS Médias Burundi

Wakaazi wa kata mbali mbali za jiji la Bujumbura waliohojiwa, wanahakikisha kuwa sasa ni zaidi ya siku tatu bila kupata hata tonya la maji kwenye ma bomba yao.

” Limekuwa ni jambo la kawaida. Ninatembea kila siku na jerikani ndani ya gari langu, ili wakati wa kurejea nyumbani niangalie wapi ninaweza kuchota maji”, alilaani mkaazi wa kata ya Gasekebuye ( kusini mwa jiji).

” Jambo la kushangaza ni kwamba sehemu ya kata hiyo inapata maji safi, wakati sehemu nyingine haina huduma hiyo. Hali hiyo imedumu kwa siku nyingi. Jambo la kusikitisha ni kuwa Regideso haina uwezo la kutoa suluhu kwa tatizo hilo ” amelalamika mkaazi wa kusini mwa jiji la Bujumbura.

Wakaazi wa kata zingine zinazokabiliwa na uhaba wa maji safi wanasema kuwa wanalazimika kulipa ili kupata baadhi ya jerikani ama dumu katika maeneo jirani.

” Jerikani moja hununiliwa franka mia mbili lakini bei inaweza kufikia elfu moja”, alibaini mkaazi mmoja.

Wakaazi wao wanasema kuwa hawana la kufanya. Wanaomba Regideso ( mamlaka ya maji ya umeme ) kutafuta suluhu la haraka na la kudumu. Wanahofia kuambukizwa maradhi yanayosababishwa na usanifishaji mdogo. Uhaba huo unakuwa tishio kubwa kwao hasusan wa wakikumbuka janga la kipindupindu.

” Hakika, janga hilo lilidhibitiwa haraka, lakini hatuwezi kukosa woga”, alieleza mkaazi mmoja wa kata ya Mutanga-Nord kaskazini mwa jiji la kibiashara.

Wanaomba ugavi wa maji ufanyike kwa usawa katika kata zote.

Upande wa Regideso, wanasema sababu kuu ya uhaba huo wa maji , ni mji unaoendelea kuwa mkubwa pamoja pia na kuzeheka kwa mitaro ya maji.

Kuhusu sababu ya kwanza Regideso haina suhulu , lakini inahakikisha kuwa wanaweka mitaro mipya katika nafasi ya ili iliyozeheka.

Previous Goma: kijana mdogo uuwawa na askali polisi katika kituo cha kuandika wapiga kura
Next Goma: mahakama ya kijeshi yaahirisha kesi ya kigogo wa Lucha