Goma: mahakama ya kijeshi yaahirisha kesi ya kigogo wa Lucha

Goma: mahakama ya kijeshi yaahirisha kesi ya kigogo wa Lucha

Kesi dhidi ya Mwamisyo Ndungo mwanaharakati ya vuguvugu la LUCHA ndani ya mkoa wa Kivu kaskazini iliotaraji kusikilizwa jumatano saa nne, iliahirishwa katika siku nyingine, korti ya kijeshi mkoani humo ilifahamisha. Mkuu wa korti hiyo alifahamisha kuwa hatua hiyo imesababishwa na kukosa uwezo wa kifedha kwa ajili ya kusafirisha mtuhumiwa. Hatua hiyo ilipingwa vikali na wenzake waliokuwa wamewasili kusikiliza kesi hiyo. HABARI SOS Médias Burundi

Wanaharakati wa Lucha wanalaani mwenendo huo ambao nia ya kumunyima mwenzao haki yake ya kuripoti mahakamani.

” Mwenzetu Mwamisyo Ndungo hakuripoti mahakamani jumatano hii kama ilivyotarajiwa. Sababu, korti ya kijeshi ya mkoa wa Kivu kaskazini ilibaini kuwa haina pesa kwa ajili ya kumusafirisha mtuhumiwa kutoka jela hadi katika ukumbi wa kusikilizia kesi. Mwenendo huo unakiuka katiba kuhusu haki yake ya kupata sheria na haraka bila kupendelea. Inaweka wazi pia nia ya viongozi wa Kongo ya kunyamanzisha wakosoaji wote wakati huu uchaguzi mkuu wa 2023 ukikaribia” alibaini Moïse Nzabara wa Lucha.

” Ni maskitiko makubwa kuona kesi iliyopangwa kusikilizwa leo na kuahirishwa katika siku nyingine bila kuwepo sababu zinazoeleweka. Ninagundua kuwa ni njama ya kumubakiza Mwamisyo ndani ya jela pasina kuripoti mahakamani “, alibaini Moïse Hangi, mwanaharakati mwingine.

” Mkuu wa korti ya kijeshi alifahamisha kuwa hana gari kwa ajili ya kumusafirisha mtuhumiwa. Tunajiuliza nauli ni ngapi kutoka Munzenze hadi mahakamani, pesa inayohitajika ni kiwango gani hadi kesi kuahirishwa. Tunalaani vikali mwenendo huo wa vyombo vya sheria dhidi ya mwenzetu Mwamisyo Ndungo. Tunaomba aachiliwe huru kwa kusubiri uamzi wa awali usimamishwe na jaji katika kesi ya rufaa” alilazimisha Baraka ambaye pia ni mfuasi wa Lucha.

Wakili wa mtuhumiwa aliwasihi kuwa na uvumilivu.

” Munafahamu kuwa vyombo vya sheria vina uhuru. Tunalazimika kuheshimu ukweli wake na hali ya nchi yetu. Mkuu wa korti ya kijeshi ameamuru kuahirisha kesi hiyo hadi wiki ijayo. Ninatumai kuwa marafiki pamoja na wajumbe wa familia ya Mwamisyo Ndungo tutapata matokeo mazuri wakati kesi itakaposikilizwa tena”, alisisitiza wakili Didier Balume.

Mwamisyo Ndungo alisimamishwa aprili 2022 na kuzuiliwa katika gereza kuu la Muzenze mjini Goma. Katika kesi ya awali alikatiwa kifungo cha miaka 5 jela kwa kosa la kukosoa serikali ya kijeshi katika mkoa wa Kivu kaskazini na Ituri tangu 2021.

Previous Bujumbura : wakaazi wasumbuka kupata maji safi
Next Burundi : shirikisho la vyama viwili vya kutetea haki za wafanyakazi vinaomba CNDS kuingilia kati katika mzozo dhidi ya serikali