Burundi : shirikisho la vyama viwili vya kutetea haki za wafanyakazi vinaomba CNDS kuingilia kati katika mzozo dhidi ya serikali
Mashirikisho ya vyama vya wafanyakazi COSYBU na CSB vinapaza sauti dhidi ya kusimamishwa kwa tozo za michango ya wajumbe wao. Serikali iliweka hatua ya kupiga marufuku michango ya wajumbe wa vyama vya wafanyakazi kuchukuliwa moja kwa moja kwenye mishahara yao. Mashirika hayo mawili yanaomba upatanishi wa kamati ya kitaifa ya mjadala wa kijamii (CNDS) ufanyike kuhusu swala hilo. HABARI SOS Médias Burundi
Kupitia malalamiko dhidi ya serikali ya Burundi yaliyowasilishwa kwa mkuu wa kamati ya kitaifa ya mjadala wa kijamii, shirikisho la vyama vya wafanyakazi COSYBU na CSB vinatoa wito, kwa niaba ya vyama vyote vya kutetea haki za wafanyakazi nchini i Burundi kwa CNDS kuunganisha pande mbili kuhusu swala la hatua ya serikali ya kusimamisha michango kuwa ilitolewa moja kwa moja kwenye mishahara ya wajumbe wa vyama hivyo.
Mashirikisho hayo mawili yanathibitisha kuwa hatua hiyo inazorotesha urasibu mzuri wa ofisi zao.
Mashirika hayo mawili yanatuhumu serikali kukiuka sheria kuhusiana na utekelezwaji wa makubaliano 87 ya OIT ( shirika la kimataifa kuhusu kazi) kuhusu uhuru wa kuunda chama cha wafanyakazi na kulinda haki ya kuunda chama cha wafanyakazi pamoja pia na makubaliano nambari 135 kuhusu kuwalinda wawakilishi wa wafanyakazi na kuwarahisishia.
Katika ziara za wajumbe wa serikali zilizofanyika kati ya januari na februari mwaka huu, waziri mkuu Gervais Ndirakobuca akiwa mkoani Makamba, alifahamisha kuwa hatua ya kutoa tozo ya michango moja kwa moja kwenye mishahara kwa ajili ya vyama vya wafanyakazi imesimamishwa.
Baadhi ya wafanyakazi walilaani kuona kuna kiwango cha pesa kilichokatwa kwenye mishahara kufadhili vyama vya ushirika ambapo sio wajumbe.
Kupitia mashtaka hayo yaliyowasilishwa tarehe 4 aprili 2023, shirikisho la vyama vya ushirika la COSYBU na CSB, hawajapinga kuwepo kwa visa vya aina hiyo lakini wanaitumu serikali kuharakisha kuchukuwa hatua ya kusitisha tozo hilo badala ya kujadili na wawakilishi wa vyama vya ushirika ili kuonyesha majukumu ya kila upande.
Mashirika hayo yanaomba mazungumzo yafanyike kumaliza mara mwisho swala kuhusu haki ya kujiunga na chama cha ushirika utekelezwaje.
You might also like
Burundi: kasisi atoa wito wa kujiuzulu kwa mamlaka zisizojali masaibu ya raia
“Mchungaji mwema ni yule anayelihurumia kundi lake zaidi.” Kikumbusho kilichotolewa Jumapili iliyopita kwenye Kanisa Kuu la Regina Mundi na Padre Viateur Ntarataze.Kasisi huyo alishutumu hotuba ya “kila kitu ki sawa”
Kuzuiliwa kwa mwandishi wa habari Sandra Muhoza – Taarifa kwa vyombo vya habari kutoka kwa wanahabari wa SOS Médias Burundi
Tunalaani vikali kuzuiliwa kiholela kwa mwenzetu, Sandra Muhoza, aliyefungwa tangu Aprili 18 mjini Bujumbura. Ukandamizaji huu wa makusudi dhidi ya vyombo huru vya habari ni dharau kwa uhuru wa kujieleza
RDC (Ituri) : angalau wananchi 40 waliuwawa na waasi wa CODECO
Vijiji vitatu vya eneo la Banyali Kilo, wilayani Djugu katika mkoa wa Ituri mashariki mwa DRC vililengwa na mashambulizi ya wakati mmoja ya waasi wa CODECO (shirikisho kwa ajili ya
