DRC : sheria kuhusu uhuru wa vyombo vya habari inataraji kutangazwa

DRC : sheria kuhusu uhuru wa vyombo vya habari inataraji kutangazwa

Waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari Patrick Muyaya alifanikisha azma yake jumanne hii mbele ya wabunge wa kitaifa. Mswada wake wa sheria kuhusu marekebisho ya sheria ya kiwaziri inayopanga utaratibu wa kutekeleza uhuru wa vyombo vya vyombo vya habari, uhuru katika kutoa habari na vipindi vya radio na televisheni, magazeti na njia zingine za mawasiliano nchini DRC uliidhinishwa na bunge la taifa. HABARI SOS Médias Burundi

Kwa mjibu wa waziri Muyaya, mswada huo wa sheria unaonyesha muono wa rais wa jamuhuri na madili ya kuwajibika kwa serikali na kuimarisha hadhi ya nchi.

Bwana Muyaya alizidi kufahamisha kuwa utafiti kuhusu hali ya uhuru wa kujieleza tayari ulifanyika.

” Tulianza zoezi hilo kwa ushirikiano na mashirika ya wandishi wa habari mbali mbali ili kuangalia hali halisi ya uhuru wa kujieleza upande mmoja na hali jumla ya vyombo vya habari katika nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha uhuru wa kujieleza”, alibaini waziri.

Licha ya upinzani wa baadhi ya wabunge wa nchi kuhusu utekelezwaji wa haraka wa sheria hiyo, waziri Muyaya alionyesha umuhimu wake ili kufikia hatua nyingine katika sekta ya vyombo vya habari nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.

” Iwapo serikali imeamuru kutoa kipau mbele kwa sheria hiyo ni kwa sababu kuna dharura. Sheria hiyo itasaidia kumaliza idadi kubwa ya matatizo yanayosumbua kila siku katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na dosari na kwenda kinyume kwa baadhi ya vyombo vya habari hususan vyombo vya mitandaoni huku teknolojia ikiendelea kwa kasi kubwa”, alisisitiza waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari.

Na kuzidi kuwa : ” Ninawaambia kuwa radio zote hazienezi vigezo. Hakuna sheria inayozihusu. Kwa hiyo hatuwezi kuchelewesha kutekeleza sheria hiyo. Kuna haja ya haraka iki kurejesha mamlaka ya serikali “.

Ikumbukwe bunge la taifa lilifanya tathmini na uidhinishwaji wa miswada mingine saba ya sheria kuhusu kurekebisha sheria za kiwaziri zilizochukuliwa katika kutoa mamlaka kwa serikali .

Previous Burundi : shirikisho la vyama viwili vya kutetea haki za wafanyakazi vinaomba CNDS kuingilia kati katika mzozo dhidi ya serikali
Next Ngozi : mfuasi wa chama cha CNL apatikana akiwa maiti

About author

You might also like

Haki za binadamu

Tanzania : biashara haramu ya watoto wa kike ambao ni wakimbizi kutoka Burundi kambini

Inashuhudia ” biashara ya wasichana wadogo” katika kambi za wakimbizi wa Burundi nchini Tanzania. Wanaolengwa zaidi ni wasichana wenye umri chini ya miaka 18. Wanaelekea hasa katika miji ya Mwanza,

Usalama

Rutana-Giharo : viongozi wa chama tawala walazimisha wapinzani kutoa michango kwa ajili ya siku kuu yao

Kulingana na mkuu wa chama cha CNL tarafani Giharo mkoa wa Rutana (kusini mashariki mwa Burundi), viongozi wa eneo hilo wa chama tawala walitoa mamlaka kwa Imbonerakure ( wajumbe wa

Utawala

Cibitoke: kwa kuhalalisha ndoa ya mwanamume aliyevalia mavazi ya karateka, afisa wa utawala alikamatwa.

Mshauri anayehusika na masuala ya utawala na kijamii wa wilaya ya Rugombo, katika mkoa wa Cibitoke (kaskazini-magharibi mwa Burundi) anazuiliwa katika seli ya kituo cha polisi cha mkoa kwa kusherehekea,