DRC : sheria kuhusu uhuru wa vyombo vya habari inataraji kutangazwa
Waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari Patrick Muyaya alifanikisha azma yake jumanne hii mbele ya wabunge wa kitaifa. Mswada wake wa sheria kuhusu marekebisho ya sheria ya kiwaziri inayopanga utaratibu wa kutekeleza uhuru wa vyombo vya vyombo vya habari, uhuru katika kutoa habari na vipindi vya radio na televisheni, magazeti na njia zingine za mawasiliano nchini DRC uliidhinishwa na bunge la taifa. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mjibu wa waziri Muyaya, mswada huo wa sheria unaonyesha muono wa rais wa jamuhuri na madili ya kuwajibika kwa serikali na kuimarisha hadhi ya nchi.
Bwana Muyaya alizidi kufahamisha kuwa utafiti kuhusu hali ya uhuru wa kujieleza tayari ulifanyika.
” Tulianza zoezi hilo kwa ushirikiano na mashirika ya wandishi wa habari mbali mbali ili kuangalia hali halisi ya uhuru wa kujieleza upande mmoja na hali jumla ya vyombo vya habari katika nchi nzima kwa lengo la kuhakikisha uhuru wa kujieleza”, alibaini waziri.
Licha ya upinzani wa baadhi ya wabunge wa nchi kuhusu utekelezwaji wa haraka wa sheria hiyo, waziri Muyaya alionyesha umuhimu wake ili kufikia hatua nyingine katika sekta ya vyombo vya habari nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo.
” Iwapo serikali imeamuru kutoa kipau mbele kwa sheria hiyo ni kwa sababu kuna dharura. Sheria hiyo itasaidia kumaliza idadi kubwa ya matatizo yanayosumbua kila siku katika sekta hiyo ikiwa ni pamoja na dosari na kwenda kinyume kwa baadhi ya vyombo vya habari hususan vyombo vya mitandaoni huku teknolojia ikiendelea kwa kasi kubwa”, alisisitiza waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari.
Na kuzidi kuwa : ” Ninawaambia kuwa radio zote hazienezi vigezo. Hakuna sheria inayozihusu. Kwa hiyo hatuwezi kuchelewesha kutekeleza sheria hiyo. Kuna haja ya haraka iki kurejesha mamlaka ya serikali “.
Ikumbukwe bunge la taifa lilifanya tathmini na uidhinishwaji wa miswada mingine saba ya sheria kuhusu kurekebisha sheria za kiwaziri zilizochukuliwa katika kutoa mamlaka kwa serikali .
You might also like
Bujumbura – Uvira: kukamatwa kwa raia wa Kongo kumezua wasiwasi
SOS Médias Burundi Bujumbura/Uvira, Juni 3, 2026 – Raia kadhaa wa Kongo wamekamatwa katika miezi ya hivi karibuni katika jiji la Uvira, Kivu Kusini, na pia Bujumbura, mji mkuu wa
Bukavu: Wawili wauawa kwa kupigwa risasi, ukosefu wa usalama haujadhibitiwa
SOS Médias Burundi Bukavu, Mei 20, 2025 – Watu wawili waliuawa na wa tatu kujeruhiwa vibaya Jumatatu jioni huko Uvira, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wakati wa
Butanyerera: Wafanyabiashara na watumishi wa umma waliolazimishwa kufadhili jeshi na Imbonerakure
SOS Médias Burundi Kirundo, Januari 8, 2026 – Tangu Jumanne iliyopita, kampeni ya kuchangisha fedha imekuwa ikiendelea katika tarafa iliopanuliwa ya Kirundo, katika jimbo la Butanyerera, kaskazini mwa Burundi. Kulingana
