Kayogoro : wafuasi wa vyama vya upinzani watiwa wasi wasi na sensa inayofanyika
Wafuasi wa vyama vya upinzani wanasema kuwa wanahofia mabaya kutokea kufuatia sensa iliyoanza jumatano tarehe 7 juni katika kijiji vyote vya tarafa ya Kayogoro mkoa wa Makamba (kusini mwa Burundi) . Sensa hiyo ya wananchi kuhusu vyama vyao inaendeshwa na wafuasi wa tawi la vijana wa chama cha CNDD-FDD Imbonerakure. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mjibu wa vyanzo katika tarafa ya Kayogoro, sensa hiyo ilianza jumatano tarehe 7 katika vijiji vyote vya tarafa hiyo.
Sensa hiyo inatofautisha wafuasi wa chama cha CNDD-FDD na wale wa upinzani, jinsia na miaka yao .
Vyanzo vyetu vinathibitisha kuwa Imbonerakure wanaofanya sensa hiyo hupita nyumba hadi nyingine katika vijiji vyote na vitongoji.
Kulingana na vyanzo katika baadhi ya Imbonerakure wanaoendesha sensa hiyo, zoezi hilo linalenga kuwatishia wafuasi wa vyama vya upinzani ili wasithubutu kuonyesha uwanachama wao katika vyama vya upinzani.
” Hiyo itatusaidia kupotosha matokeo ya uchaguzi ujao”, walihakikisha Imbonerakure waliozungumza na SOS Médias Burundi.
” Hiyo itatuwezesha kuhakikisha kuwa hakuna hata mfuasi mmoja wa chama cha upinzani katika vijiji mbali mbali na kwa hiyo chama cha upinzani hakitakuwa na haki ya kupinga matokeo” alifahamisha Imbonerakure mmoja wa eneo hilo kwa sharti ya kubana jina lake.
Upande wa upinzani, wafuasi wanasema kuwa wanaishi katika hali ya wasi wasi kwa sababu ” hali hiyo inaweza kusababisha mauwaji ya wafuasi wa upinzani”.
Wanaomba viongozi wa nchi kusimamisha mara moja aina hiyo ya sensa. Viongozi wa tarafa na wakuu wa chama tawala hawakupatikana ili kujibu maswali yetu.
You might also like
Burundi : nchi imeorodheshwa katika nchi za kwanza ambako rushwa imekithiri
Maadhimisho ya siku ya Afrika dhidi ya rushwa tarehe 11 julai 2023 : hakuna maendeleo makubwa kwa mujibu wa OLUCOME (shirika la kupambana na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya
Miaka Mitano Madarakani nchini Burundi: Rais Ndayishimiye asherehekea “ushindi wake juu ya upinzani” katika maombi huko Gitega
SOS Médias Burundi Gitega, Juni 21, 2025 — Miaka mitano baada ya kuingia mamlakani, Rais Évariste Ndayishimiye alisherehekea ukumbusho wake ofisini huko Gitega kwa vita vya kidini vilivyojaa jumbe za
Burunga: Mvuvi aliyeuawa na kiboko kwenye ufukwe wa ziwa Tanganyika
SOS Médias Burundi Rumonge, Septemba 7, 2025 – Msiba ulitokea Jumamosi usiku kwenye mwambao wa Ziwa Tanganyika. Mwili usio na uhai wa mvuvi uligunduliwa mapema asubuhi ya Septemba 7, si
