Uvira : watu wawili wauwawa
Watu hao ni wanaume wawili wa jamii ya Banyamulenge. Waliuwawa na watu wanaobebelea silaha ambao wanadaiwa kuwa ni waasi wa kundi la Mai Mai jumapili hii alasiri. Kisa kilitokea katika eneo la Kirungu, wilayani Uvira mkoa wa Kivu kaskazini mashariki mwa DRC. HABARI SOS Médias Burundi
Wahanga hao walikuwa wakitoka katika mji wa Uvira wakielekea eneo la Minembwe huku wakitumia barabara ya Uvira-Kirungu-Bijombo.
Ruyenzi Kavuganyi alikuwa mkaazi wa kitongoji cha Bizimana wakati ambapo Rigean Rumaraninda akiishi katika kitongoji cha Nyabigugu.
Waliuwawa na watu wenye silaha ambao walidaiwa kuwa waasi wa kundi la Mai Mai-Makanaki.
” Watu hao wawili waliuwawa wakati wakitembea na miguu. Waasi waliowamalizia maisha, walikuwa wakivalia sare za jeshi la FARDC ( jeshi la jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo)”, mashahidi wamesema.
Kwenye barabara hiyo, angalau watu 5 wajumbe wa jamii ya Banyamulenge waliuwawa na watu wa makundi ya silaha ya ndani kwa mjibu wa mwakilishi wa shirika moja la eneo hilo.
” Ni jambo la kusikitisha na mauwaji hayo ninayachukuwa kama mauwaji ya kuvizia sababu ni watu wa jamii ya Banyamulenge wanaolengwa wakati ambapo Bafulero, Bashi, Bavira wanaosafiri pamoja nao, wakiwa hawaguswi “, analaani Musore, msafiri anayetumia barabara ya Uvira-Kirungo-Bijombo.
” Pamoja na hayo, watu hao wameuwawa wakiwa karibu na kizuwizi cha wanajeshi. Mara nyingi, wanauwawa baada ya kuwalipa wanajeshi lakini wanajeshi hao hawawashindikizi kwa ajili ya kuwalinda”, vyanzo vyetu viliendea kwa sharti ya kuhifadhi majina yao. Wahanga hao wa siku ya jumapili waliuwawa karibu ya kizuwizi cha jeshi.
Watu wengine wawili walijeruhiwa wakati wa shambulio hilo la jumapili dhidi ya wasafiri hao wawili. Majeruhiwa ni askali polisi wawili wajumbe wa jamii ya Banyamulenge pia.
Rutabara Sengambi na Rugazura walikuwa hawana silaha wakati walipovamiwa”, vyanzo vyetu vinasema.
Msemaji wa jeshi la FARDC katika jimbo la Kivu kusini hakupatikana ili kujibu maswali yetu kadhalika yule wa kundi la Mai Mai-Makanaki.
Kati ya 2017 na 2022, angalau wajumbe wa jamii ya Banyamulenge 1500 waliuwawa nchini Kongo kwa mujibu wa wanaharakati wanaotetea haki za watu wa jamii hiyo ambao kwa sehemu kubwa inaundwa na wafugaji.
Wanaharakati hao wanasema kuwa ” Mauwaji hayo yanachukuwa mueleko wa mauwaji ya kikabila kuelekea mauwaji ya kuangamiza ama jenoside”.
You might also like
Dzaleka (Malawi): ukosefu wa usalama, wasiwasi kwa kila mtu
Ripoti kutoka kwa uchunguzi wa UNHCR kuhusu sababu za kuongezeka kwa uhalifu katika kambi ya Dzaleka imetangazwa hadharani ndani ya kambi hiyo. Hati hiyo inapendekeza kwamba wahalifu lazima wapatikane na
Ukandamizaji, umaskini, propaganda: Ligi ya Iteka yatoa hati ya mashtaka dhidi ya utawala wa Ndayishimiye
SOS Médias Burundi Bujumbura, Agosti 8, 2025 — Alipoingia mamlakani Juni 2020, kufuatia kifo kisichotarajiwa cha mtangulizi wake Pierre Nkurunziza, Évariste Ndayishimiye aliibua matumaini. Matumaini ya maisha mapya, mapumziko na
Nyarugusu (Tanzania) : mauwaji ya mkimbizi kutoka Kongo anayetuhumiwa kuwa mwanachama wa kundi la M23
Ni mwanaume ambaye aliwasili hivi karibuni katika kambi ya Nyarugusu. Aliuwawa asubuhi ya alhamisi hii. Watu wenye silaha wanaovalia sare za polisi na za kawaida walimuuwa mkimbizi huyo kutoka Kongo
