DRC – Rutshuru : usalama wazidi kuwa mbaya katika kitongoji cha Busanza
Wakaazi wa kitongoji cha Busanza ndani ya kijiji cha Bwisha wilayani Rutshuru mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo walaani kuona visa vya usalama mdogo vikiendelea kushuhudiwa mnamo siku hizi katika baadhi ya maeneo ambako kunaripotiwa waasi wa M23 na makundi ya silaha ya ndani. Vyanzo mbali mbali vinasema kuwa uwepo wa makundi hayo mawili yanayozozana, huchangia katika kuleta hali ya usalama mdogo ndani ya maeneo hayo. HABARI SOS Médias Burundi
Kwa mujibu wa vyanzo eneo hilo, mapigano kati ya kundi la M23 na makundi ya silaha na waasi eneo hilo yanafanyika takriban kila siku. Baadhi ya wananchi hukimbia na kwenda nchini Uganda wakati wengine wakielekea kwenye makao makuu ya wilaya ya Rutshuru.
” Kutokana na hali hiyo, shughuli za kijamii na kiuchumi zilisimama tangu miezi kadhaa. Mbali na hayo, maeneo hasa ya : Ruharashi, Kaitorea, Changwi, Kitagoma na Kavugizo yanaathiriwa zaidi na visa vya ubakaji, wizi wa mali, utekaji nyara dhidi ya wananchi. Wakimbizi wa ndani ” wanadai kuwa serikali ya Kongo iliwasahau “.
Wakimbizi hao wanaoishi kwenye mpaka baina ya Kongo na Uganda wanaomba viongozi wenye nguvu kuhusishwa ili amani iweze kurudi katika maeneo hayo ya mkoa wa Kivu kaskazini.
You might also like
Kivu Kusini: Wanajeshi wa Burundi kwa wingi Fizi kupunguza mwendo wa Twirwaneho na kuwadhibiti M23
SOS Media Burundi Bukavu, Mei 22, 2025 – Harakati kubwa za kijeshi zimezingatiwa katika siku za hivi majuzi mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tangu Jumatano, wanajeshi wapya wa
Mipaka Iliyofungwa, maisha yaliyovunjwa: hali ya watu wa kaskazini mwa Burundi
SOS Médias Burundi Butanyerera, Julai 9, 2025 – Kufungwa kwa muda mrefu kwa mpaka kati ya Burundi na Rwanda kunaendelea kutumbukiza mikoa ya mpakani ya kaskazini mwa nchi hiyo katika
Kaburantwa – DRC: Misafara ya wanajeshi wa Burundi wakielekea Kivu Kusini, huku kukiwa na mvutano wa kikanda na kimya rasmi
SOS Médias Burundi Bujumbura, Septemba 2, 2025 — Kwa muda wa siku tatu, misafara mizito ya wanajeshi wa Burundi imekuwa ikipitia mji wa Kaburantwa, katika eneo la Cibitoke mkoani Bujumbura,
