Burundi : ni mapema kubainika wazi madhambi ya Bunyoni

Burundi : ni mapema kubainika wazi madhambi ya Bunyoni

Mahakama kuu ya Burundi alhamisi hii ilifahamisha kuwa mwendeshamashtaka mkuu wa jamuhuri anaendelea kutafuta mashtaka mapya dhidi ya Bunyoni. Msemaji wa mahakama kuu na ofisi ya mwendeshamashtaka mkuu aliyefahamisha hayo, alizidi kusema kuwa mwendeshamashtaka yuko na taarifa mpya zinazoweza kumuelekeza kwenye njia ya maovu mengine katika faili dhidi ya waziri mkuu wa zamani Allain Guillaume Bunyoni. HABARI SOS Médias Burundi

Ni katika kipindi cha wasemaji wa taasisi za umma ambapo msemaji wa mwendeshamashtaka mkuu alifahamisha hayo. Alikuwa akijibu swali la mwandishi wa habari wa ndani ya nchi.

“Katika awamu wa mwanzo, Bunyoni alifuatiliwa kwa kuvuruga usalama wa ndani ya nchi, kuhujumu uchumi na kutumia cheo chake kutafuta maslahi yake binafsi na kumiliki silaha kinyume cha sheria pamoja na kumutukana rais wa nchi”, alifahamisha Agnès Bangiricenge.

Alisema kuwa “mwendeshamashtaka alikataa rufaa baada ya wakili wake kupinga hatua ya kumushikilia jela kwa muda. Mwendeshamashtaka alipata habari mpya zinazoweza kumufungulia mashtaka mapya”, alisisitiza.

Mmoja kati ya waendeshaji wa kipindi alitaka kujuwa maelezo zaidi kuhusu madai ya kumiliki silaha kinyume cha sheria wakati Bunyoni akiwa askali polisi wa cheo cha jemedali.

“Ni wewe unaoona hivyo na kusema hivyo hivyo. Iwapo wamesema anamiliki silaha kinyume cha sheria, inamaanisha kuwa waligundua nyumbani kwake silaha zingine mbali na zile anazoruhusiwa kumiliki”, alijibu hivyo kwa hasira.

Mwanzoni mwa mwezi mei mwaka huu, Alain Guillaume Bunyoni alipelekwa katika gereza kuu ya Ngozi (Kaskazini mwa Burundi) baada ya kumaliza siku nyingi katika gereza la SNR (idara ya kitaifa ya ujasusi) ndani ya mji wa kibiashara wa Bujumbura.

Shirika la Human Right Watch linaomba viongozi wa Burundi kuhakikisha kesi dhidi yake inaendeshwa kwa haki na uwepo wa waangalizi wa kimataifa ili haki ya Bunyoni iweze kuheshimiwa”.

Muasi huyo wa zamani wa kihutu chini ya vikwazo vya serikali ya marekani, alifutwa kwenye wadhifa wake na rais wa jamuhuri Evariste Ndayishimiye mwanzoni mwa mwezi septemba 2022 katika mazingira ya giza.

Previous Kayogoro : hali ya wasi wasi yawakabili wananchi kutokana na mazoezi ya kijeshi ya Imbonerakure
Next Burundi : tatizo la uhaba wa mafuta, majibu yake bado kupatikana

You might also like

Utawala

Kilimo cha chai nchini Burundi: Hekta 1,300 zimeachwa au kuharibiwa; uzalishaji washuka kwa asilimia 30

SOS Médias Burundi Kayanza, Septemba 7, 2026—Uzalishaji wa chai nchini Burundi umeshuka kwa asilimia 30 katika muongo uliopita, hasa kutokana na ukosefu wa motisha miongoni mwa wakulima pamoja na uhaba

Utawala

Kirundo: Wafanyakazi wa tarafa wafungwa jela kwa tuhuma za ubadhirifu wa kodi

SOS Médias Burundi Kirundo, Aprili 23, 2026 – Katika tarafa ya Kirundo, katika mkoa wa Butanyerera, kaskazini mwa Burundi, kesi ya madai ya ubadhirifu wa fedha za umma inatikisa utawala

Utawala

Burunga: Mgogoro wa mbolea wageuka kuwa jinamizi, wakulima wahofia janga la chakula

SOS Médias Burundi Bururi, Juni 22, 2026 – Wakati kilimo kikisalia kuwa chanzo kikuu cha maisha kwa sehemu kubwa ya wakazi wa mashambani, wakulima katika tarafa za Matana na Bururi,