Burundi : bei ya tiketi ya usafiri yapanda
Waziri wa biashara alitangaza jumatano hii bei mpya na nauli ya usafiri ndani ya mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura na katika ya mikoa. Bei ya tiketi ndani basi mjini Bujumbura popote pale unapotoka na kuelekea kati kati mwa mji ilipandishwa franka 50 sarafu za Burundi. Kati kati mwa nchi nauli itapanda kwa franka 500. HABARI SOS Médias Burundi
Waziri Marie Chantal Nijimbere alifahamisha kupitia tangazo kuwa bei ya nauli za usafiri ilipandishwa kutokana na kupanda kwa bei ya mafuta ya gari tangu jumatatu hii.
Wakaazi wa jiji la Bujumbura walibaini kuwa walitaraji ongezeko hilo la bei ya tiketi litatokea.
” Bila shaka na bei ya vyakula na bidhaa zingine mahitajio muhimu zitapanda”. wanalaani wakaazi wengine ambao wanazidi kuwa walitupiliwa “.
Wengine wanasema kuwa hawaelewi malengo ya serikali. Wafanyakazi wa umma wanasema kuwa serikali inalenga kukusanya pesa iliyotumia katika kutekeleza sera ya kusawazisha mishahara iliyoanza kutelelezwa tangu julai iliyopita”.
” Bei ya bidhaa muhimu itapanda pia kwa mkondo huo”, wanalaani wafanyakazi wa serikali.
Bei ya tiketi ya usafiri ilipanda mara ya mwisho katika mwezi julai iliyopita.
Hatua hiyo ilisababisha bei ya bidhaa zingine kama sukari, simenti na vinywaji kupanda licha ya kuendelea kuadimika kwenye soko nchini Burundi.
You might also like
Bujumbura: kukamatwa na kufuatiwa na kuwekwa kizuizini kwa maafisa wa kampuni ya kibiashara na utengenezaji
Meneja mkuu wa kampuni ya biashara na utengenezaji bidhaa iliyoko Bujumbura, jiji la kibiashara la Burundi, na msaidizi wake wamekuwa wapangaji wa gereza kuu la Bujumbura linalojulikana kwa jina la
Burundi : tatizo la uhaba wa mafuta, majibu yake bado kupatikana
Baada ya miezi 18 ya uhaba wa mafuta ya gari, viongozi wa Burundi hawawapi moyo wananchi. Wanachukuwa hatua zisizodumu. Wanaharakati upande wao, wanaomba mkutano mkuu ufanyike kuhusiana na tatizo hilo.
Bujumbura: bei ya tikiti ya basi imeongezeka mara tatu kaskazini mwa ukumbi wa jiji
Wasafirishaji wanaendelea kukisia bei ya tikiti za usafiri katika sehemu ya kaskazini ya mji mkuu wa kiuchumi Bujumbura. Kwa kawaida, bei ya tikiti ya usafiri kwenye sehemu ya katikati ya
