Bujumbura : kazi zavurugika kutokana na umeme unaokatika mara kwa mara
Hali ya umeme kukatika mara kwa mara inaripotiwa katika mji mkuu wa kiuchumi wa Bujumbura. Wakaazi wanalalamika huku wafanyabiashara wanaoendesha shughuli za kibiashara wakidai kupata hasara kubwa. Mamlaka ya maji na umeme Regideso bad o haijatoa maelezo. HABARI SOS Medias Burundi
Ni wengi wanaolalamika kutokana na hali hiyo ya umeme kukatika mara kwa mara ndani ya mji wa Bujumbura.
” Tunalazimika kulipa franka elfu moja za ziada kwenye gharama ya kushevu nywele. Ni pesa nyingi wakati uchumi wa nchi ukiwa mbaya “, aliambia SOS Medias Burundi akiwa na hasira mwanamke mmoja aliyekuwa akitoka katika chumba cha kutengeneza nywele za wanawake.
Wanaofanya kazi ya kuchevu nywele wanasema kuwa hali hiyo huwaletea shida na wateja wao sababu hawaelewi tatizo la kutumia mafuta ya gari. Ni bidhaa inayonunuliwa kwa franka nyingi”.
Katika mgahawa wa vyakula pembeni, mrasibu analaani hasara aliyopata katika wiki mbili zilizopita.
” Tunanunua chakula ambacho kitatumiwa kwa siku moja. Ni muda wa asubuhi ambapo tunapata matatizo mengi sababu hatuwezi kuuzisha maziwa. Tulikuwa na uwezo wa kuuzisha hadi lita 15 kwa siku lakini tunalangua tu lita tano ili kujiepusha na hasara ” alihakikisha.
Katika familia ambazo zina mazoea ya kununua vitu vinavyohidhiwa ndani ya frije au jakofu, bidhaa hizo zinaoza siku moja badaye.
Kwa mjibu wa ushuhuda uliotolewa na wandishi wetu, umeme unakatika kwa angalau mara nne kwa siku kabla ya kukatika kwa muda mrefu wakati wa usiku.
” Hatuelewi umuhimu wa Regideso “, wanalaani.
Regideso bado haijajieleza kuhusiana na madai hayo ya wakaazi.
You might also like
Kodi ya angani katika miji mikuu ya Burundi: mgogoro wa kimya kimya unaozinyonga kaya
SOS Médias Burundi Bujumbura, Aprili 29, 2025 – Tangu mwaka jana, ukodishaji wa nyumba katika miji mikuu ya Burundi, ikiwa ni pamoja na Bujumbura, Gitega, na Ngozi, umeongezeka, wakati mwingine
Bubanza: kupanda kwa bei ya bidhaa za Brarudi, utawala wa ndani unakejeli watumiaji
Bei za bidhaa za Brarudi (viwanda vya bia vya Burundi na ndimu) zinaendelea kuongezeka katika wilaya na jimbo la Bubanza (magharibi mwa Burundi). Wateja wa bidhaa hizi wanaomba uongozi wa
Burundi : nchi imeorodheshwa katika nchi za kwanza ambako rushwa imekithiri
Maadhimisho ya siku ya Afrika dhidi ya rushwa tarehe 11 julai 2023 : hakuna maendeleo makubwa kwa mujibu wa OLUCOME (shirika la kupambana na vitendo vya rushwa na matumizi mabaya
