Gitega : hakuna sheria miaka 27 baada ya mauwaji ya askofu Joachim Ruhuna

Gitega : hakuna sheria miaka 27 baada ya mauwaji ya askofu Joachim Ruhuna

Askofu Joachim Ruhuna mkuu zamani wa dayosezi ya Gitega aliuwawa tarehe 9 septemba 1996. Mauwaji hayo yalifanyika karibu na mto wa Mubarazi. Katika kipindi hicho, maeneo ya Bugendana na Mutaho katika mkoa wa Gitega na Gihogazi ndani ya mkoa wa Karusi mashariki ya kati mwa Burundi yalikuwa chini ya udhibiti ya waasi wa kundi la FDD, ambacho sasa ni chama tawala cha CNDD-FDD. Miaka 27 baada ya mauwaji yake, familia inaomba sheria ichukuwe mkondo wake. HABARI SOS Médias Burundi

Katika sherehe kwa niaba ya hayati askofu Ruhuna zamani mkuu wa dayosezi ya Gitega zilizofanyika katika parokia ya Mumuri, umati mkubwa ulihudhuria sherehe hizo.

Katika mahubiri yake, askofu Jean Marie Harushimana padri wa parokia ya Shatanya aliyeongoza ibada hiyo ya misa, alifahamisha kuwa askofu Ruhuna hakuwahi kuogopa kumwaga damu yake kwa ajili amani nchini Burundi “.

” Katika siku ambapo aliuwawa tarehe 9 septemba 1996, alikuwa amepata taarifa hizo na walimusihi asichukuwi njia ya Bugendana-Mutaho, lakini aliamuru kufanya ziara ya kuhamasisha amani katika parokia na vituo cha wakimbizi wa ndani “, alikumbusha.

Askofu Jean Marie Harushimana alihubiri msamaha, upendo, umoja, maridhiano na kuishi kwa amani, tabia ambazo hayati Joachim Ruhuna alikuwa akitoa kipau mbele. Alisisitiza pia juu ya haki za binadamu na kuomba warundi kuacha ubaguzi na kulipiza kisasi.

Mwanadini atakayekumbukwa daima

Hayati askofu Joachim Ruhuna atakumbukwa daima katika mioyo ya wakaazi wa mji wa Gitega ( mji mkuu wa kisiasa).

Katika mzozo wa 1993 uliosababishwa na mauwaji ya Melchior Ndadaye, rais wa kwanza wa kabila ya wahutu aliyechaguliwa kidemokrasia mwaka huo, wakati akiwa wa kabila ya watutsi, askofu alikusanya wasomi na wafanyabiashara wa Kabila la kihutu ndani ya majengo ya parokia hiyo ili kuwalinda dhidi ya vijana wauwaji na jeshi la kabila moja la watutsi “.

Ushuhuda mwingine

Mwezi julai iliyopita, tume ya ukweli na maridhiano (CVR) ilikusanya manusura wa mauwaji wa 1972 yaliyosababisha vifo vya wahutu wengi kuliko wa tutsi. Lengo lilikuwa kutambua ” mashujaa “. Kati ya manusura hao ni pamoja na wakili Fabien Segatwa, mmoja kati ya mawakili watetezi wa zamani nchini Burundi na barani Afrika. Uhai wake uliokolewa na maaskofu wawili wa kanisa katoliki. Hao ni pamoja na askofu mkuu wa zamani wa Gitega ( kati kati mwa Burundi) Johachim Ruhuna aliuwawa katika mwaka wa 1996 na watu wanaobebelea silaha waliodaiwa kuwa waasi wa kundi la FDD, kikundi cha zamani cha waasi wa kihutu kilichogeuka chama tawala tangu 2005 kutokana na makubaliano ya amani ya Arusha ya mwaka wa 2000, pamoja na askofu wa zamani wa dayosezi ya Bujumbura Evariste Ngoyagoye ambaye yuko katika mapumziko ya uzeeni.

” Watumishi wa kweli wa Mungu wanatofautiana na watu wengine. Hakuna anayeweza kusema kuwa hayati askofu Ruhuna au Ngoyagoye walifanya hivyo kwa kutegemea chochote kutoka kwangu. Seminari kubwa ya Bujumbura ( mji mkuu wa kibiashara) ilituonyesha mfano kuwa binadamu anaweza kutekeleza wajibu wake”, alitoa ushuhuda huo mmoja kati ya mawakili maarufu katika nchi hii ndogo ya Afrika mashariki.

Kulingana na wakili Segatwa ni budi ” watu wafahamu kuwa makaazi ya askofu wa zamani wa Gitega Ruhuna yalikuwa daima eneo la maficho kwa watu wanaokimbia kifo”.

Tarehe 9 septemba ya kila mwaka, uongozi wa kanisa katoliki mkoa wa Gitega ilichagua siku hiyo kama siku maluum ya msamaha na maridhiano.

Tarehe 23 julai 1996 askofu mkuu wa zamani wa Gitega alikuwa alidai kuwa ” walipata laana ” waasi ambao waliwauwa raia 648 wa Kabila la watutsi katika kambi ya Bugendana. Shambulio hilo lilidaiwa kutekelezwa na waasi wa FDD. Wahanga walikuwa walinusurika mauwaji yaliyofanyika baada ya kifo cha rais wa kwanza wa Kabila la bahutu alichaguliwa kidemokrasia Melchior Ndadaye na kuuwawa mwezi oktoba 1993. Mwaka wa 1996, kwa niaba ya kanisa katoliki nchini Burundi, mkuu wa zamani wa baraza la maaskofu wa kanisa katoliki nchini Burundi askofu Bernard Bududira alituhumu wazi waasi wa FDD kuwa walimuuwa mwanadini huyo. Watu wengine wawili akiwemo mtawa mmoja wa kanisa katoliki waliokuwa pamoja na askofu huyo ndani ya gari waliuwawa pia.

Previous DRC (Mulongwe) : wakimbizi wanaotafuta kuuni za kupikia waathiriwa na ubakaji
Next Burundi : bei ya mafuta ya gari yapanda kwa mara ya pili katika kipindi cha miezi miwili