DRC (Mulongwe) : wakimbizi wanaotafuta kuuni za kupikia waathiriwa na ubakaji

DRC (Mulongwe) : wakimbizi wanaotafuta kuuni za kupikia waathiriwa na ubakaji

Katika kambi ya wakimbizi wa Mulongwe ndani ya mkoa wa Kivu kusini mashariki mwa jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo, wakimbizi wanakabiliwa na ukosefu wa kuuni za kupikia. Wakimbizi hao hususan akinamama na wasichana wanakwenda hadi katika misitu ya karibu kutafuta kuuni. Kwa mjibu wa vyanzo kutoka viongozi katika jamii, wengi wao wanabakwa na watu wanaobebelea silaha na kunyanganywa simu zao pamoja na vifaa vya kukata kuni. HABARI SOS Médias Burundi

Kulingana na vyanzo ndani ya kambi, akinamama wakimbizi wanakwenda kutafuta kuuni ndani ya misitu ya Kaseke na Katalukulu. Ni katika misitu hiyo ambapo wanawakuta wanaume wanaobebelea silaha kama alivyofahamisha B.Marie mama wa watoto watano.

” Tunatembea kwa takriban kilometa 6 na miguu. Baadhi yetu wanabakwa ndani ya msitu huku wengine wakinyanganywa simu zao”.

Habari hizo zinathibitishwa na Deo Ntakirutimana kiongozi wa wakimbizi wenye uraia wa Burundi ndani ya kambi ya Mulongwe.

Kwa mjibu wake, kuna watu wanaoingia musituni kutafuta kuuni za kupikia lakini wanakuta matatizo hasa ubakaji.

Kutokana na ukosefu wa kuuni za kupikia, baadhi ya wakimbizi wanatumia nyasi ili kupika chakula.

Kambi ya wakimbizi ya Mulongwe inawapa hifadhi zaidi ya wakimbizi kutoka Burundi elfu 10.

Previous Cibitoke : wafungwa wawili wafariki wakiwa katika gereza la polisi ya mkoa
Next Gitega : hakuna sheria miaka 27 baada ya mauwaji ya askofu Joachim Ruhuna