Rumonge : vijana wazuiliwa kuingia nchini Tanzania na DRC kwa hofu ya kwenda kujiunga na makundi ya silaha
Kwa kipindi cha wiki tatu sasa, ni marufuku kwa warundi kuingia nchini Jamuhuri ya kidemokrasia ya Kongo na Tanzania. Vijana wanatuhumiwa kutaka kujiunga na makundi ya silaha ya warundi yanayopatikana nje ya nchi hususan nchini RDC. Wahusika wanadai ni ukiukwaji wa haki na uhuru wa kutembea. HABARI SOS Médias Burundi
Katazo hilo kwa wasafiri halikuandikwa rasmi kwa mjibu wa vyanzo vyetu mkoani Rumonge.
” Hatua hiyo halikubandikwa. Lakini polisi ya mpakani inayokaguwa nenda rudi kwenye bandari ya Rumonge haikubali kijana wa kiume yoyote kuvuka, na hali hiyo ni tangu wiki tatu zilizopita”, mashahidi wanasema.
Amri hiyo huenda ilitolewa na viongozi wakuu wa nchi kulingana na vyanzo vya polisi.
Vijana wanatuhumiwa kwenda kujiunga na makundi ya silaha ya Burundi yaliyopiga kambi nchini DRC. Kwa wale ambao wana nia ya kwenda nchini Tanzania sababu za kuwakataza hazikutangazwa.
Mkoani Rumonge, wakaazi wanalaani kuwa huo ni ukiukwaji wa uhuru wa kutembea. Wanadai kuwa hatua hiyo ina madhara makubwa katika biashara na maendeleo.
[…], vijana wasio na ajira walikuwa wakielekea kila siku nchini Tanzania kwa ajili ya kuomba vibarua ndani ya mashamba. Na wanaporudi wanakuwa na pesa ndogo ya kujisaidia. Lakini angalia namna wanavyowakataza kwenda. Hatua hiyo haina umuhimu wowote, alidai mkaazi mmoja.
Kwa mjibu wa vyanzo vya polisi, hatua hiyo unasababishwa na tuhuma za uwepo wa vijana wanaokwenda kujiunga na makundi ya waasi.
“[….], Iliripotiwa kuwa vijana wa Burundi wenye asili ya mikoa ya Ngozi, Kirundo (kaskazini) na Muyinga ( kaskazini-mashariki) wanakwenda kwa wingi nchini DRC. Wanawatuhumu kwenda kujiunga na kundi la silaha la Burundi nchini DRC hata kama hakuna uhakika, vyanzo vyetu vinasema.
Viongozi wa mikoa hadi sasa hawatoa maelezo kamili kuhusiana na faili hiyo.
You might also like
Bujumbura : young shopkeepers forced to close to attend CNDD-FDD meetings
SOS Médias Burundi Bujumbura, February 12, 2026 – Young people working in shops, hair saloons, and cafes in the Jabe neighborhood, in the Bwiza zone of the Mukaza district in
Bujumbura: a chaotic results collection, the opposition calls for rerun of polls
Bujumbura, June 8, 2025 — Following the legislative and district elections of June 5, the new province of Bujumbura (western Burundi) has been rocked by a series of disturbing revelations
Beni: thirteen civilians killed by Ugandan ADF rebels
Thirteen bodies of civilians were discovered in crop fields on Wednesday in the Bashu chiefdom, Beni territory, in the province ofNorth Kivu, eastern DRC. According to local sources who provided
