Zambia : karibu warundi 30 wanazuiliwa jela kwa kosa la uhamiaji haramu
Polisi nchini Zambia inafahamisha kuwa iliwakamata raia kutoka Burundi 29 kwa kosa la uhamiaji haramu. Walipitia Tanzania na lengo lao lilikuwa kufika nchini Afrika ya kusini. Wanaharakati wanasema ni biashara ya watu na kuomba viongozi wa Burundi kuchukuwa hatua ili kuzuia mwenendo huo ambao umekuwa mnamo siku hizi. HABARI SOS Médias Burundi
Operesheni ya kuwakamata warundi hao iliendeshwa na polisi baada ya kupewa taarifa ya idara ya uhamiaji.
” Operesheni hiyo ya pamoja iliwezesha polisi kuwakamata watu 29 wanaotuhumiwa kosa la uhamiaji haramu ambao ni wenye asili ya Burundi. Watuhumiwa wako na umri kati ya miaka 10 na 40″, aliwambia wandishi wa habari wa ndani Josephine Malambo afisa wa mawasiliano kwenye idara ya uhamiaji nchini Zambia.
” Watu 12 wenye asili ya Burundi waliingia nchini Zambia kwa kukaguliwa na idara ya uhamiaji ya Zombe, 13 ambao walikuwa na karatasi bandia za usafiri waliingia nchini Zambia kupitia Mbala wakati wengine walikuwa hawana kataratasi hata moja. Wote wanazuiliwa katika kanda ya Chirundu kwa ajili ya uchunguzi”, alizidi kusema.
Wote waliingia nchini Zambia mwezi januari uliopita.
Biashara haramu ya watu…….
“Shirika la ONLCT où est ton frère ?”, ni shirika linalopinga biashara haramu ya watu, linatahadharisha. Polisi ya Uganda iliwakatama watu wengine wenye asili ya Burundi 24 waliokuwa wakielekea katika nchi wa warabu mwezi huu.
” Zaidi ya warundi 50 walisimamishwa katika kipindi cha mwezi mmoja kwa kosa la uhamiaji haramu katika nchi za ukanda huu! Sio jambo la kawaida” alisema wakili Prime Mbarubukeye, kiongozi wa shirika hilo ambaye anazidi kuwa ni ” biashara haramu ya watu inayoendelezwa”.
Shirika jingine linalopigana dhidi ya uhalifu wa kuvuka mipaka linaeleza kuhusu sababu za ongezeko la warundi kuelekea katika nchi za kigeni.
” Ni kutokana na umasikini, ukosefu wa ajira unaoongezeka na ukosefu wa mitaji hususan kwa vijana, ugavi mbaya wa vitambulisho vya usafiri kama pasipoti pamoja pia na mpango wa kuwatuma wafanyakazi nje ambapo unatekelezwa vibaya na haujulikani kwa wengine”.
ONLCT où est ton frère inaomba serikali ya Burundi kuzingatia tatizo hilo na kuona kama ni tatizo kubwa.
” Serikali inatakiwa kuandaa vizuri huduma ya utaoaji wa vitambulisho vya usafiri ili viweze kupatikana kwa muda na kufuatilia kwa karibu swala la uhamiaji haramu wa warundi nchini Zambia ambao unaaanza kuleta wasi wasi kama ilivyokuwa nchini Serbia. Serikali inatakiwa kusaini makubaliano ya kupeana wafanyakazi na nchi za afrika ambako kuna fursa nyingi kama Zambia, afrika ya kusini, Tanzania, Uganda na Kenya…… kama ilivyofanya na nchi za Saudia Arabia. Inatakiwa pia kufanya programu za ajira ili kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana ” anashahuri bwana Mbarubukeye.
Wanaharakati wanahofia kuwa wahamiaji haramu wanaweza kuwa chanzo cha usalama mdogo ndani ya nchi jirani.
About author
You might also like
Tanzania: UNHCR reaffirms support for refugees
The UNHCR Country Representative in Tanzania is visiting refugee camps across the country. She reassured them of their permanent support this year. Both in Nyarugusu and in Nduta, Mahoua Parums,
Meheba (Zambia) : dozens of houses destroyed by torrential rains
The months of December and January are the rainiest in Zambia, especially in the northwestern part which is home to the Meheba refugee camp. The latter has already recorded several
Mahama (Rwanda): a young Burundian refugee found dead
Lazare Ndayishimiye, 25, was found dead, his body decomposing in his room this Friday. At least five suspects were arrested following the macabre discovery which occured at Mahama camp located