Kivu-Kaskazini: serikali ya Kongo imepandisha idadi ya waliouwawa eneo la Kishishe

Kivu-Kaskazini: serikali ya Kongo imepandisha idadi ya waliouwawa eneo la Kishishe

Idadi ya waliuwawa eneo la kitongoji cha Kishishe, ndani ya wilaya ya Rutshuru, kivu-kaskazini mashariki mwa DRC ilipanda. Baada ya kupatikana kwa miili mingine, sasa ni vifo vya watu 272 wakiwemo watoto 17. Serikali ya Kongo siku ya jumatatu ilifahamisha kuwa uchunguzi ulianzishwa na kuna nia ya kupeleka mashtaka kwenye mahakama ya ICC (Mahakama ya uhalifu wa kivita). M23 upande wake, linasema ni mchezo unaofanywa ili kupuzia maovu mengine yaliyofanyika katika eneo hilo na vikosi vya serikali pamoja na washirika wake”. HABARI SOS Médias Burundi

Idadi hiyo bado ni ya muda, kulingana na vyanzo vya ndani sababu watu wengine bado hawajapatikana ikizingatiwa kuwa maeneo mengi yako chini ya udhibiti wa M23, viongozi wa Kongo wakiwa hawawezi kuwasili maeneo hayo.

Idadi hiyo ilitangazwa na gavana wa zamani wa Kivu kaskazini Julien Paluku waziri wa sasa wa viwanda. Ilikuwa katika kikao na wandishi wa habari jumatatu hii tarehe 5 disemba 2022 mjini Kinshasa, mji mkuu wa DRC.

Waziri wa mawasiliano na vyombo vya habari ambaye pia ni msemaji wa serikali Patrick Muyaya, alifahamisha kuwa uchunguzi wa kimataifa ulianzishwa ili waliofanya mauwaji hayo wachukuliwe hatua mbele ya sheria”.
Msemaji wa serikali ya Kongo aliwaambia wandishi wa habari kuwa ” waziri wa sheria yuko mjini the Hague nchini uholanzi kukutana na mwendeshamashtaka wa korti kuu ya kimataifa (ICC) kwa sababu hiyo.

” Waziri wa sheria yuko ziarani mjini the Hague ili kukutana na mwendeshamashtaka. Alitoa amri kwa mwendeshamashtaka ili faili ifunguliwe. Kwa hiyo uchunguzi tayari ulianzishwa”, alisema.

Na kuzidi kuwa ” waziri wa sheria ambaye yuko mjini the Hague atakutana na mwendeshamashtaka sababu anataka uchunguzi uanzishwe ili mwanga wote upatikane kuhusu mkasa huo “.

Mashirika ya kiraia ya ndani na vyanzo vingine vinahakikisha kuwa zaidi ya miili 300 ya raia wa kawaida waliouwawa ilipatikana katika maeneo mengi karibu na Kishishe.

Viongozi wa kundi la M23 walitupilia mbali madai hayo na kusema kuwa :” ni mchezo ili kuwafanya watu kusahawu maovu mengine yaliyofanywa na jeshi la taifa na washirika wake katika eneo hilo”. Tangu mauwaji hayo kutangazwa wiki moja iliyopita, wajumbe wa kundi la M23 walitupilia mbali madai hayo, na kuyataja kama ” uongo ambao malengo yake ni kuwaharibia uhusiano wao na wananchi na kuomba uchunguzi huru ufanyike”.

Kundi la machi 23 waasi hao wa zamani wa kabila la watutsi walichukuwa silaha tena mwishoni mwa mwaka wa 2021, wakutuhumu serikali ya Kongo kutoheshimu ahadi yao kuhusu kuwarudisha katika maisha ya kawaida wapiganaji wa kundi hilo. Viongozi wa Kongo wanaendelea kutuhumu Rwanda kuunga mkono waasi hao. Mwishoni mwa juma, rais wa Kongo Félix Tshisekedi alituhumu moja kwa moja mwenzake wa Rwanda Paul Kagame kuwa ” adui wa DRC”. Serikali ya Rwanda alipinga madai hayo.

Ingawa kundi la M23 nina wawakilishi wengi na kudhibiti maeneo mengi katika mkoa wa Kivu kaskazini likiwemo eneo la Bunagana, mji wa mpakani na Uganda tangu mwishoni mwa juni mwaka huu, halikualikwa katika awamu ya tatu ya mazungumzo ya Nairobi yaliyopangwa kuhitimishwa jumatatu hii. Mmoja kati ya wasemaji wa kundi hilo Canesius Karemera Munyarugo hivi karibuni aliambia gazeti la SOS Médias Burundi kuwa ” matokeo ya mkutano huo yanawahusu wale walioalikwa”.

Hata hivyo makundi mengine ya silaha yaliyoshiriki katika kikao yanahakikisha kuwa hayana mpango wa kuweka silaha chini.

” Hatutaweka silaha chini. Hatuogopi kikosi cha kikanda na hatuna usalama. Hadi sasa ni miaka zaidi ya 20 tukiwa hatuna amani wakati ambapo Monusco iko hapa, majeshi ya Kongo na Uganda yaliungana…..tutaweka silaha chini wakati ambapo makundi hayo ya nje ya nchi yatakuwa yamefurushwa nje ya Kongo”, alifahamisha Aimable Nabulizi msemaji wa kundi Mai Mai Bilozebishambuke linalowajibika eneo la kivu-kusini.

Serikali ya Kongo hivi karibuni alitoa tahadhari kwa makundi yote ya waasi ambayo hayataweka silaha chini baada ya mazungumzo ya Nairobi kuwa ” yanajikokotea hasira ya kikosi cha kikanda”, jambo ambalo haliogopwi na waasi hao wanaosema kuwa ” tunapigana kujihami na Kupigania jamii zetu”.

Previous Bujumbura: a woman's corpse discovered
Next Nyanza-Lac: viongozi wawili wa chama cha CNDD-FDD wafukuzwa nje ya chama

About author

You might also like

Security

Kayokwe : two women detained for infanticide

Irakoze Josiane, 19 years old, is detained in the cell of the Kayokwe district police station in Mwaro province (central Burundi). She is accused of killing the baby she gave

Security

Ngozi : two people killed in one night

Two people were killed during the night from Monday to Tuesday in the districts of Ngozi and Ruhororo (Ngozi province, northern Burundi). One of the victims has been identified while

Human Rights

Mzozo mashariki mwa Kongo : askali mmoja wa kikosi cha umoja wa mataifa auwawa na mwingine kujeruhiwa vikali kutokana na shambulizi dhidi ya ndege la Monusco

Monusco (ujumbe wa umoja wa mataifa nchini DRC) umetangaza kifo cha askali wake kupitia tangazo. Ujumbe huo unafahamisha kuwa alifariki kutokana na shambulio dhidi ya moja kati ya ndege zake